Sujuud ni dalili kubwa kabisa ya mja kujidhalilisha mbele ya Mola wake ( ́Azza wa Jall). Hapo mja ameviweka viungo vitukufu, takasifu na vilivyo juu kabisa vya mwili wake kwenye udongo na kujivunjavunja. Zaidi ya hayo inafuatiwa kujivunjavunja kwa moyo, kujishusha na kumnyenyekea Allaah ( ́Azza wa Jall). Kwa ajili hiyo ikawa malipo ya muumini anapoyafanya hayo ni Allaah ( ́Azza wa Jall) kumkurubisha Kwake. Imesihi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake pale anaposujudu. Hivyo ombeni du´aa kwa wingi.”[1]
Allaah (Ta´ala) amesema:
وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب
”… basi sujudu na kurubia!”[2]
Isitoshe Sujuud ni kitendo ambacho washirikina walikuwa wakimfanyia kiburi Allaah ( ́Azza wa Jall). Baadhi walisema kwamba wanachukizwa kusujudu kwa sababu misuli ya makalio yao itakuwa juu zaidi kuliko nyuso zao. Wengine walikuwa wakitosheka kuchukua mikononi mwao kiganja cha changarawe na wanakipandisha kwenye vipaji vya nyuso zao. Allaah alimfukuza Ibliys baada ya kukataa kumsujudia Aadam. Kwa ajili hiyo analia pale muumini anaposujudu na husema:
”Mwanadamu ameamrishwa kusujudu ambapo akafanya hivyo na hivyo anapewa Pepo. Niliamrishwa kusujudu ambapo nikaasi na hivyo napewa Moto.”[3]
[1] Muslim (482).
[2] 96:19
[3] Muslim (81).
- Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 76-77
- Imechapishwa: 24/11/2025
Sujuud ni dalili kubwa kabisa ya mja kujidhalilisha mbele ya Mola wake ( ́Azza wa Jall). Hapo mja ameviweka viungo vitukufu, takasifu na vilivyo juu kabisa vya mwili wake kwenye udongo na kujivunjavunja. Zaidi ya hayo inafuatiwa kujivunjavunja kwa moyo, kujishusha na kumnyenyekea Allaah ( ́Azza wa Jall). Kwa ajili hiyo ikawa malipo ya muumini anapoyafanya hayo ni Allaah ( ́Azza wa Jall) kumkurubisha Kwake. Imesihi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake pale anaposujudu. Hivyo ombeni du´aa kwa wingi.”[1]
Allaah (Ta´ala) amesema:
وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب
”… basi sujudu na kurubia!”[2]
Isitoshe Sujuud ni kitendo ambacho washirikina walikuwa wakimfanyia kiburi Allaah ( ́Azza wa Jall). Baadhi walisema kwamba wanachukizwa kusujudu kwa sababu misuli ya makalio yao itakuwa juu zaidi kuliko nyuso zao. Wengine walikuwa wakitosheka kuchukua mikononi mwao kiganja cha changarawe na wanakipandisha kwenye vipaji vya nyuso zao. Allaah alimfukuza Ibliys baada ya kukataa kumsujudia Aadam. Kwa ajili hiyo analia pale muumini anaposujudu na husema:
”Mwanadamu ameamrishwa kusujudu ambapo akafanya hivyo na hivyo anapewa Pepo. Niliamrishwa kusujudu ambapo nikaasi na hivyo napewa Moto.”[3]
[1] Muslim (482).
[2] 96:19
[3] Muslim (81).
Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 76-77
Imechapishwa: 24/11/2025
https://firqatunnajia.com/19-sujuud-inafahamisha-unyenyekevu/