19. Ni wajibu kumkumbusha mwenye kula au kunywa mchana wa Ramadhaan kwa kusahau

2- Anayemuona mwenye kula au kunywa mchana wa Ramadhaan hali ya kusahau ilihali amefunga ni lazima kwake kumkumbusha. Haijuzu kwake kumnyamazia kama wanavofikiria baadhi ya watu wajinga. Kwa sababu kufanya hivo ni katika kuamrisha mema na kukataza maovu. Jengine ni kwa sababu kula na kunywa mchana wa Ramadhaan ni maovu. Mwenye kusahau anapewa udhuru. Lakini ni lazima kumkumbusha. Kwani kufanya hivo ni katika kusaidizana katika wema na kumcha Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswaru fiy Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 33
  • Imechapishwa: 23/05/2019