Shubuha ya tatu: Wako wenye kudai kwamba ulinganizi wetu juu ya kufuata Sunnah na kutochukua maoni ya maimamu yanayokwenda kinyume na Sunnah hiyo kwamba hiyo maana yake ni kwamba sisi tunaacha kabisa kuyachukua maoni yao na kutofaidika na Ijtihaad zao zao.
Madai haya yako mbali kabisa na usawa vile inavowezekana. Ni waziwazi kwamba ni batili. Yale yote niliyoyataja mpaka sasa yanafahamisha kinyume chake kabisa. Yale ninayolingania ni kwamba watu wasiyafanye madhehebu kuwa ni dini badala ya Qur-aan na Sunnah. Kwa njia ya kwamba watu wakawa ni wenye kurejea katika madhehebu wakati wa mizozo. Haitakiwi kurejea katika madhehebu ili kufikia hukumu mpya zinazohusiana na matukio ya leo, kama wanavofanya baadhi. Kutokana na madhehebu wameweka hukumu mpyampya zinazotumiwa katika hali za kibinafsi, ndoa, talaka na mengineyo. Badala yake walitakiwa kurejea katika Qur-aan na Sunnah ili kupambanua kati ya jambo la sawa na la makosa, haki na batili. Watu hawa wanatendea kazi matamshi kama kutofautiana kwa Ummah ni rehema, kuchukua ruhusa, kufanya wepesi au yale wanayoita kuwa ni ´maslahi`. Ni uzuri ulioje wa yale maneno yaliyosemwa na Sulaymaan at-Taymiy (Rahimahu Allaah):
“Yule mwenye kuchukua ruhusa za wanachuoni wote ulimwenguni anakusanya shari yote.”
Ameipokea Ibn ´Abdil-Barr ambaye amesema:
“Haya ni kwa maafikiano. Sijui kama kuna ambaye alionelea kinyume.”[1]
Haya ndio tunayokemea. Kama unavyoona mwenyewe kuna maafikiano juu yake.
Kuhusu kurejea katika maoni yao, kufaidika nayo na kutaka msaada kwayo katika kuifahamu haki katika yale mambo ambayo kuna tofauti juu yake na mambo ambayo hakuna dalili ya wazi katika Qur-aan na Sunnah au mambo ambayo kuna haja ya kuwekwa wazi zaidi, mimi sipindi jambo hilo. Bali tunaliamrisha na kulishaji´isha. Yule mwenye kuongozwa na Qur-aan na Sunnah bila shaka hufaidika kwayo. ´Allaamah Ibn ´Abdil-Barr (Rahimahu Allaah) amesema:
“Ni lazima kwako kuhifadhi misingi na kuitilia umuhimu. Tambua ya kwamba yule mwenye kujibidisha kuhifadhi Sunnah na hukumu za Qur-aan na akadurusu maoni ya wanachuoni ili ziweze kumsaidia katika Ijtihaad yake, akatafakari na kufafanua ile Sunnah ambayo inaweza kuwa na maana nyingi (na sio kwa sababu ya kumfuata kichwa mchunga yeyote katika wao kama ambavyo Sunnah inatakiwa kufuatwa kwa hali zote), akahifadhi na kuzingatia juu ya Sunnah kama wafanyavyo wanachuoni, akachukua utafiti wao, uelewa wao na mitazamo yao, akawashukuru kutokana na juhudi zao alizofaidika nazo, akawasifia kwa yale maoni yao waliyopatia (ambako ndio mara nyingi) na asiwatake kutokamana na kukosea (kama ambavo wao wenyewe hawakufanya hivo) – ndiye mwanafunzi ambaye ameshikamana na mfumo wa as-Salaf as-Swaalih. Ni mwenye kupatia, mwenye kuona ukomavu wake na mwenye kufuata njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake.”
Yule mwenye kuacha kutafakari, akapuuzilia mbali yale niliyoyataja na akayapa kipaumbele maoni yake kabla ya Sunnah basi huyo ni mpotevu mwenye kupoteza wengine. Na yule ambaye si mwenye kuyajua yote hayo na akachukua fatwa bila ya elimu ni kipofu na mwenye kupotea zaidi.”[2]
Hii ni haki, isiyokuwa na utatizi
achana na mimi kutokamana njia za vichochoro
[1] Ibn ´Abdil-Barr katika ”al-Jaamiy´” (2/91-92).
[2] Ibn ´Abdil-Barr katika ”al-Jaamiy´” (2/172).
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 61-63
- Imechapishwa: 23/01/2019

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 61-63
Imechapishwa: 23/01/2019
https://firqatunnajia.com/19-msimamo-wetu-juu-ya-maoni-ya-maimamu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)