7 – Upokezi wa ´Abdullaah bin Naafiy´[1]

Haafidhw Ibn ´Abdil-Barr (Rahimahu Allaah) amesema: Abu Muhammad ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Abdil-Mu´miyn ametukhabarisha: Ahmad bin Ja’far bin Hamdaan bin Maalik ametuhadithia: ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal[2]  ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: Surayj bin an-Nu´maan[3] ametuhadithia: ´Abdullaah bin Naafiy´ ametuhadithia:

“Allaah (´Azza wa Jall)  yuko juu ya mbingu na ujuzi Wake upo kila mahali. Hakuna mahali unakosekana.” Ikasemwa kuambiwa Maalik:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[4]

Amelingana juu vipi?” Maalik (Rahimahu Allaah) akasema: “Kulingana Kwake kunafahamika na namna haifahamiki. Kuuliza kwako juu ya hili ni Bid´ah na nakuona ni mtu muovu.”[5]

[1] Watu wawili kwa jina hili wamepokea kutoka kwa Maalik: Mmoja wao Abdullaah bin Naafiy’ bin as-Swaa-igh, aliyefariki mwaka 206, na mwengine ni ´Abdullaah bin Naafiy’, mjumuu wa Thaabit bin ´Abdillaah bin az-Zubayr bin al-Awwaam az-Zubayr, ambaye pia anatambulika kama ´Abdullaah bin Naafiy’ as-Swaghiyr, ambaye alifariki mwaka 216. Haikunibainikia ni nani kati ya wawili hao anayemkusudia hapa. adh-Dhahabiy amesema:

“Si mara chache wanazuoni kuyachananya mapokezi yao. Bali uhakika wa mambo ni kwamba wengi hawajui kwamba wao ni watu wawili tofauti.” (Siyar A´lâm-in-Nubalaa’ (10/372))

Kabla ya hapo alinukuu al-Qaadhwiy ´Iyaadhw, ambaye amemnukuu Suhnuun ambaye alikuwa anaona kuwa ni wajibu kuwabainisha mabwana hao wawili, ingawa wote walikuwa madhubuti, ili mapokezi yao yasichanganyike. Amesema:

“as-Swaa-igh alikuwa ni mkubwa, aliyetangulia na imara zaidi inapokuja kwa Maalik, kwa sababu ya kule kutangamana naye kwa kipindi kirefu.”

Amesema kuhusu az-Zubayriy ya kwamba alikuwa mkweli. Hakuna shida kubwa katika suala hilo. Masimulizi kutoka kwa wote mawili hayashuki chini ya kiwango cha kuwa nzuri.

[2] Mtoto wa Imamu wa Ahl-us-Sunnah Ahmad bin Hanbal. adh-Dhahabiy amesema juu yake:

“Imaam, mwenye kuhifadhi na mwenye kujeruhi. Muhaddith wa Baghdad, Abu ´Abdir-Rahmaan, mwana wa Shaykh wa zama Abu ´Abdillaah.” (Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (13/375))

al-Khatwiyb amesema:

“Alikuwa wa madhubuti, thabiti na mwenye ufahamu.” (Taarikh Baghdaad (9/375))

Alikufa mnamo 290.

[3] Surayj bin an-Nu´maan bin Marwaan al-Jawhariy al-Lu’lu-iy, Abul-Husayn, kwa jina jingine Abul-Hasan, al-Baghdaadiy. Alikuwa madhubuti kwa mujibu wa Yahyaa bin Ma´iyn, al-´Ijliy na Abu Daawuud na wengineo. Ibn Hajar amesema juu yake:

“Mwaminifu ambaye wakati mwingine hukosea kidogo.” (Taqriyb-ut-Taqriyb)

Alifariki mnamo 217. Tazama “Tahdhiyb-ul-Kamaal” (10/218) ya al-Mizziy.

[4] 20:05

[5] at-Tamhiyd (7/138).  Makusudio ya kwamba Kulingana Kwake kunafahamika kunamaanishwa ile maana yake, kama yalivyotilia nguvu yale mapokezi mengine pamoja na jumla isemayo ”namna haifahamiki”.

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 37-39
  • Imechapishwa: 29/11/2025