Aina ya pili ya misingi ya tofauti za tafsiri ni ile inayojulikana kwa kutumia dalili na si kwa kutumia mapokezi. Makosa mengi katika aina hii yanatokana na pande mbili zilizojitokeza baada ya tafsiri za Maswahabah, wanafunzi wao na wale waliowafuata kwa wema. Tafsiri za Qur-aan zinazotegemea maneno ya pande hizi mbili zinakaribia kutokuwa na makosa, kama vile tafsiri ya ´Abdur-Razzaaq, ya Wakiy´, ya ´Abd bin Humayd, ya ´Abdur-Rahmaan bin Ibraahiym bin Duhaym, ya Imaam Ahmad, ya Ishaaq bin Raahuuyah, ya Baqiyy bin Makhlad, ya Abu Bakr bin al-Mundhir, ya Sufyaan bin ´Uyaynah, ya Sunayd, ya Ibn Jariyr, ya Ibn Abiy Haatim, ya Abu Sa´iyd al-Ashajj, ya Abu ´Abdillaah bin Maajah na ya Ibn Marduuyah.
Upande mmoja ni kwamba wametilia umuhimu maana kisha baadaye wakajaribu kuyatumia matamshi ya Qur-aan kwenye maana hizo. Upande mwingine wametilia umuhimu kila kinachowezekana kwa mujibu wa lugha ya kiarabu pasi na kuzingatia ni nani ameitamka Qur-aan, imeteremshwa kwa nani na inamzungumzisha nani.
Wale wa upande wa kwanza wametilia umuhimu zile maana wanazoona pasi na kuzingatia yale majulisho na ubainifu ambao yanastahiki matamshi ya Qur-aan. Wanachojali ni yale matamshi na kinachowezekana kwa mujibu wa lugha ya kiarabu pasi na kuzingatia kile ambacho ni cha mzungumzaji na muktadha.
Isitoshe mara nyingi hawa hukosea pindi wanapoyatumia matamshi kwa maana ya ile lugha, kama walivyokosea pia wale wa mwanzo. Vilevile wa mwanzo mara nyingi hukosea katika usahihi wa maana waliyoitafsiri kwayo Qur-aan, kama wanavyokosea wale wengine. Ingawa wale wa mwanzo hutilia manani zaidi maana na wale wengine hutilia manani zaidi matamshi.
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 71-73
- Imechapishwa: 02/04/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)