03 – Kukata nywele

Miongoni mwa makosa yanayokiuka Shari´ah ni kupunguza nywele kwa njia inayofanana na nywele za wanawake wa kikafiri au nywele za wanaume, jambo ambalo halijuzu kwa mujibu wa Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wanaojifananisha na wanaume. Hukumu ni hiyohiyo pale ambapo akipunguza katika mtindo ambao unafanana na nywele za wanawake waovu, wanawake malaya na wanawake wa kikafiri, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yeyote mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”[1]

Miongoni mwa hayo kunaingia pia yale yanayoitwa ukataji wa (الكاريه). Maana yake ni kukata nywele zote na kuziacha zikafika mpaka kwenye masikio. Huo ni mtindo wa kimarekani.

[1] Abu Daawuud katika ”as-Sunan”. Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´ (02/105) nr. 6149.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 15/02/2026