78 – Ahmad bin Muhammad bin Ahmad al-Mujahhiz ametukhabarisha: Abul-Fadhwl ´Ubaydullaah bin ´Abdir-Rahmaan az-Zuhriy ametuhadithia kwa njia ya kutusomea: Ibraahiym bin ´Abdillaah bin Ayyuub al-Mukharramiy ametuhadithia: Nimemsikia Sarriy bin al-Mughallis as-Saqatwiy akisema:

”Kila unavyojiongezea elimu ndivo unavyozidisha hoja dhidi yako.”

79 – Abul-Hasan ´Aliy bin Twalhah bin Muhammad al-Muqriy ametukhabarisha: Nimemsikia Abul-Husayn Muhammad bin Ahmad bin Sam´uun al-Waa´idhw akisema:

”Elimu ni hoja na adhabu juu ya kila mmoja ambaye anaacha kuitazama ili kujua ni haki ipi alionayo Allaah kwake.”

80 – Abu Twaahir ´Abdul-Ghaffaar bin Muhammad bin Ja´far al-Mu-addib ametukhabarisha: Abu ´Aliy Muhammad bin Ahmad bin al-Hasan as-Swawwaaf ametuzindua: ´Abdullaah bin Ahmad ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: Sayyaar bin Haatim ametuhadithia: Ja´far bin Sulaymaan adh-Dhwab´iy ametuhadithia, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah siku ya Qiyaamah atawasamehe wale wasiokuwa kutokana na mambo ambayo hatowasamehe kwayo wanazuoni.” [1]

81 – Nilisoma kwenye jalada la kitabu cha Abu Bakr Muhammad bin ´Abdillaah bin Abaan al-Hiytiy:

Ikiwa elimu hauifanyii kazi kwa matendo basi inakuwa

ni hoja dhidi yako na wala hupewi udhuru kwa yale unayojua

Ikiwa unayajua haya basi unatakiwa kutambua

kuwa maneno ya mtu yanatiwa nguvu na yale anayoyatenda

[1] Hadiyth ni dhaifu na inapingana na zilizo Swahiyh kwa sababu ya Sayyaar Abu Haatim. adh-Dhahabiy amemtaja katika ”ad-Dhwu´afaa” na akataja kwamba al-Qazwiyniy amesema: ”Alikuwa pamoja nami dukani. Hakuwa na akili.” Kukasemwa: ”Je, unamtuhumu?” Akasema: ”Hapana.” Wengine wamesema kuwa ni mkweli na undani wake umesalimika. Ibn-ul-Madiyniy na wengine wamemdhoofisha.

Hadiyth imepokelewa pia na Abu Nu´aym katika “Hilyat-ul-Awliyaa’” kupitia kwa Muhammad bin Ahmad bin al-Hasan. Abu Bakr al-Marruudhiy pia ameipokea katika “al-War´”, ar-Raamhurmuziy katika “al-Faaswil”, Ibn ´Asaakir katika “Dhammu man laa ya´mal bi ´Ilmih” na adh-Dhwiyaa’ al-Maqdisiy katika “al-Ahaadiyth al-Mukhtaarah” kupitia kwa Ahmad. Abu Nu´aym amesema:

”Hadiyth hii ni geni. Sayyaar amepwekeka katika kuisimulia kutoka kwa Ja´far. Hatukuiandika isipokuwa tu kutoka katika Hadiyth za Ahmad bin Hanbal.”

Amesema mahali pengine:

”´Abdullaah amesema: ”Baba yangu amesema: ”Hadiyth hii ni dhaifu na yenye kupingana na zilizo Swahiyh. Hakunihadithia nayo isipokuwa tu mara moja.”

Pengine ndio sababu iliyomfanya kutoitaja katika ”al-Musnad”. Nukuu hiyohiyo imetajwa kutoka kwa ´Abdullaah imetajwa na adh-Dhwiyaa´ baada ya Hadiyth, na kwa ajili hiyo inastaajabisha kuona ameitaja katika ”al-Mukhtaarah”. Ibn Qudaamah ameitaja katika ”al-Muntakhab” na akasema baada yake:

”al-Marruudhiy amesema: ”Abu ´Abdillaah amesema: ”Kosa ni lenye kutoka kwa Ja´far, na si kutoka kwa Sayyaar.”

Hivi ndivo alivosema imamu. Ja´far ni bora kuliko Sayyaar. Inatosha kwamba Muslim amemjengea hoja katika yale mapokezi ya mwanzo – na Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 53-55
  • Imechapishwa: 12/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy