Swali 19: Kuna vijana wengi wanaosikiliza kanda za Salmaan al-´Awdah, Safar al-Hawaaliy, Sa´iyd al-Qahtwaaniy na ´Aaidh al-Qarniy. Je, unawanasihi vijana hawa kusitisha kusikiliza kanda zao au hapana?
Jibu: Ndio. Kwa sababu kanda zao inaweza kuwa na mambo wasiyoyajua vijana hawa na hatimaye wakadanganyika nayo. Watu hawa wana maneno yasiyokuwa mazuri. Ni maneno wanayotakiwa kuacha na wajirudi kwayo. ´Aaidh al-Qarniy – Allaah amuwafikishe na amthibitishe – amejirudi katika mambo kumi na saba. Tunatarajia vilevile atajirudi katika makosa yaliyobaki. Amesema:
Swali na ufunge utakavyo
dini haitambui mtu kwa kuswali na kufunga
Wewe ni padiri katika watawa
na sio katika watu wa Muhammad – inatosheleza kulaumika.
Haya ni mashairi ambayo kwa hakika hayatakiwi kusikilizwa. Anaamrisha kuwafanyia uasi watawala. Tunatarajia kuwa amejirudi kwayo.
Mfano wa maneno kama haya, maneno ya Salmaan na baadhi ya maneno ya Safar yanaweza kuwa na makosa ambayo hakuna mwenye kuyajua isipokuwa wanachuoni.
Lililo bora kwa mwanafunzi mwerevu asisikilize kanda hizi.
- Muhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
- Imechapishwa: 16/07/2017
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)