19. Hadiyth “Itafuteni saa ambayo inatarajiwa siku ya ijumaa… “

701- Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Itafuteni saa ambayo inatarajiwa siku ya ijumaa baada ya swalah ya ´Aswr mpaka jua kuzama.”[1]

Ameipokea at-Tirmidhiy na akasema:

“Hadiyth ni geni.”

Ameipokea vilevile at-Twabaraaniy kupitia upokezi wa Ibn Lahiy´ah na mwishoni kuna nyongeza isemeyo:

“Kiwango hichi.”

 Bi maana kiwango cha kukamata na mkono. Mlolongo wa wapokezi wake  ni Swahiyh zaidi kuliko wa at-Tirmidhiy.

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/438)
  • Imechapishwa: 13/01/2018