Swali 19: Je, inafaa kwa mtu kukusanya na kufupisha wakati wa swalah ukiingia yuko katika hali ya uenyeji kisha akasafiri kabla ya kutekeleza swalah hiyo? Vivyo hivyo kwa mfano akiswali Dhuhr na ´Aswr kwa kufupisha na kukusanya kisha akafika mjini mwake wakati wa ´Aswr – je, kitendo chake hicho ni sahihi? Wakati wa kukusanya na kufupisha alikuwa anajua kuwa atafika katika mji wake katika wakati wa swalah ya pili[1].
Jibu: Ukiingia kwa msafiri wakati wa swalah ilihali yuko mjini mwake kisha akasafiri kabla ya kuswali, basi imesuniwa kwake kufupisha pale atapoyaacha majengo ya mji wake kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Isitoshe haya ndio maoni ya jopo la wanazuoni wengi. Akikusanya na akafupisha safarini kisha akafika mjini mwake kabla ya kuingia wakati wa swalah ya pili au katika ule wakati wa pili, basi hatolazimika kuirudia kwa sababu ameitekeleza swalah kwa njia inayokubalika katika Shari´ah. Akiswali swalah hiyo ya pili pamoja na wengine basi itazingatiwa ni swalah ya sunnah.
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/290-291).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 36
- Imechapishwa: 02/03/2022
Swali 19: Je, inafaa kwa mtu kukusanya na kufupisha wakati wa swalah ukiingia yuko katika hali ya uenyeji kisha akasafiri kabla ya kutekeleza swalah hiyo? Vivyo hivyo kwa mfano akiswali Dhuhr na ´Aswr kwa kufupisha na kukusanya kisha akafika mjini mwake wakati wa ´Aswr – je, kitendo chake hicho ni sahihi? Wakati wa kukusanya na kufupisha alikuwa anajua kuwa atafika katika mji wake katika wakati wa swalah ya pili[1].
Jibu: Ukiingia kwa msafiri wakati wa swalah ilihali yuko mjini mwake kisha akasafiri kabla ya kuswali, basi imesuniwa kwake kufupisha pale atapoyaacha majengo ya mji wake kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Isitoshe haya ndio maoni ya jopo la wanazuoni wengi. Akikusanya na akafupisha safarini kisha akafika mjini mwake kabla ya kuingia wakati wa swalah ya pili au katika ule wakati wa pili, basi hatolazimika kuirudia kwa sababu ameitekeleza swalah kwa njia inayokubalika katika Shari´ah. Akiswali swalah hiyo ya pili pamoja na wengine basi itazingatiwa ni swalah ya sunnah.
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/290-291).
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 36
Imechapishwa: 02/03/2022
https://firqatunnajia.com/19-amefupishe-na-akusanye-msafiri-ambaye-wakati-wa-swalah-umeingia-kabla-ya-kusafiri/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)