19. Allaah ametutumia Mtume ili atuonyeshe namna ya kumwabudu Yeye

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Bali amewatumia Mtume;

MAELEZO

Pale ilipokuwa haijuzu kufanya ´ibaadah kwa yale ambayo sisi tumeona kuwa ni mazuri au kumfuata kibubusa mtu fulani katika watu  ndipo Allaah akatutumia Mitume ili watubainishie namna ya kumwabudu. Yote hayo ni kwa sababu ´ibaadah ni jambo la ukomekaji. Kwa msemo mwingine ni kwamba haijuzu kumwabudu Allaah kwa chochote isipokuwa yale aliyoyaweka katika Shari´ah.

´Ibaadah imekomeka kwa yale waliyokuja nayo Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Hekima ya kutumilizwa Mitume ni ili wawabainishie watu ni vipi watamwabudu Mola wao na kuwakataza kutokamana na shirki na kumkufuru Allaah (´Azza wa Jall). Hii ndio kazi ya Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Kwa ajili hii amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[1]

´Ibaadah ni jambo la kukomeka. Bid´ah ni yenye kurudishwa. Kufuata kibubusa ni jambo lenye kukataliwa. ´Ibaadah hazichukuliwi isipokuwa kutoka katika Shari´ah walizokuja nazo Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Maneno yake:

“Bali amewatumia Mtume.”

Ambaye ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yeye ndiye Mtume wa mwisho. Amemtuma ili atubainishie ni kwa nini ametuumba, atubainishie ni namna gani tutamwabudu Allaah (´Azza wa Jall), atukataze kutokamana na shirki, kufuru na maasi. Hii ndio kazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amefikisha ufikishaji wa wazi, ametekeleza amana na ameunasihi Ummah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amebainisha na kuweka wazi na pia ametuacha katika njia ya wazi kabisa; usiku wake ni kama mchana wake na hapotei kutoka humo isipokuwa anayestahiki maangamivu. Haya ni kama ilivyotajwa katika maneno Yake (Ta´ala):

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

 “Leo wamekata tamaa wale waliokufuru juu ya dini yenu, hivyo basi msiwaogope na niogopeni Mimi. Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni Uislamu uwe dini yenu.”[2]

[1] al-Bukhaariy (7350) hali ya kuiwekea taaliki na Muslim (18) (1718).

[2] 05:03

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 45-47
  • Imechapishwa: 01/12/2020