25- Halafu Shari´ah yenye hekima imejaalia alama za wazi ambazo kwazo watu wanaweza kutumia kama dalilili juu ya mwisho mwema – Allaah (Ta´ala) ametuandikia nazo kwa fadhilah na neema Zake – mtu yeyote atakayekufa kwa moja wapo basi itakuwa ni bishara nzuri kwake. Nazo ni kama zifuatazo:

1- Kutamka kwake shahaadah wakati wa kufa. Kuhusu hilo kuna Hadiyth zifuatazo:

A- “Yule ambaye maneno yake ya mwisho itakuwa ni “Laa ilaaha Allaaha illa Allaah” ataingia Peponi.”

Ameipokea al-Haakim na wengineo kwa cheni ya wapokezi nzuri kupitia kwa Mu´aadh.

Kupitia njia nyingine tena kutoka kwake kwa tamko:

“Hakuna nafsi yoyote inayokufa ilihali ni yenye kushuhudia kwamba “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba mimi ni Mtume wa Allaah” hilo linarejea katika moyo wenye yakini isipokuwa Allaah ataisamehe.”

Ameipokea Ibn Maajah, Ahmad na wengineo. Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan. Cheni ya wapokezi wake ni nzuri kwa mtazamo wangu. Hayo nimeyabainisha katika “as-Swahiyhah” (2278).

Vilevile ina ushahidi kutoka katika Hadiyth ya Abu Hurayrah iliotangulia katika “Kutamkisha shahaadah”. Kipengele cha 1 ukurasa wa 10.

B- Twalhah bin ´Ubaydillaah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwa kusema:

“Siku moja ´Umar alimwona Twalhah bin ´Ubaydillaah akiwa ni mzito na ni mwenye simanzi ambapo akasema: “Una nini, ee babake fulani? Pengine mke wa ami yako amekufanyia vibaya?” Akasema: “Hapana – [akamsifia Abu Bakr]. Isipokuwa mimi nimesikia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maneno ambayo hakuna kilichonizuia kumuuliza juu yake isipokuwa tu kushindwa kumuhoji mpaka akafariki. Siku moja niliwahi kumsikia akisema: “Hakika mimi najua maneno ambayo hatoyasema mja wakati wa kufa kwake isipokuwa itamng´azia rangi yake na Allaah atamfanyia wepesi kutoa kwake roho.” ´Umar akasema: “Mimi nayajua ni yepi.” Akamuuliza: “Ni yepi?” Akasema: “Je, hivi unayajua maneno ambayo ni makubwa zaidi kuliko yale aliyomwamrisha ami yake wakati alipotaka kufa “Laa ilaaha illa Allaah”?” Twalhah akasema: “Umesema kweli. Ninaapa kwa Allaah kwamba ni hayo.”

Ameipokea Imaam Ahmad (1384) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh, Ibn Hibbaan (02) amepokea mfano wake, al-Haakim (01/350,351) na ziada ni yake. al-Haakim amesema: “Ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim.” ad-Dhahabiy ameafikiana naye.

Kuhusiana na maudhui haya zipo Hadiyth zilizotajwa katika “Kutamkisha shahaadah”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 48-49
  • Imechapishwa: 08/01/2020