Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
143 – Kheri na shari ni mambo yamekadiriwa kwa viumbe.
MAELEZO
Makadirio ni jambo limekwishatangulia. Kuamini makadirio, kama tulivyotangulia kusema huko nyuma, ni moja katika nguzo sita za imani.Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, siku ya Mwisho na kuamini Qadar, kheri na shari yake.”[1]
Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amechukua maana hii kutoka katika Hadiyth. Kheri na shari inakuwa kwa makadirio ya Allaah (´Azza wa Jall). Hakuna chochote kinachotokea katika ulimwengu huu isipokuwa ni kutokana na mipango na makadirio ya Allaah. Ni lazima kuamini jambo hilo. Allaah (´Azza wa Jall) ameumba kheri na shari kutokana na hekima:
وَنَبْلُوكُم بِالشَّرِّ وَالْخَيْرِ فِتْنَةً ۖ وَإِلَيْنَا تُرْجَعُونَ
“Tutakujaribuni kwa mitihani ya shari na kheri na Kwetu mtarejeshwa.”[2]
Kwa njia hiyo ndio wanapambanuka waumini, wapwekeshaji na watu wanaomnyenyekea Allaah kutokana na makafiri, washirikina na wakanamungu. Kusingelikuwepo kheri basi kusingelipatikana upambanuzi.
Allaah anaipenda kheri, anaiumba na kuikadiria. Allaah anaichukia shari, lakini anaiumba na kuikadiria kutokana na hekima, kwa ajili ya kujaribu na kutahini. Isingelikuwepo shari basi kusingetokea ukafiri na kuwajengea uadui Manabii na Mitume. Isingelikuwepo kheri basi kusingelitokea jihaad, kuamrisha mema na kukataza maovu na kupenda na kuchukia kwa ajili ya Allaah. Kwa maana nyingine kusingekuwa na tofauti kati ya watu. Pengine mtu akapinga na kuhoji endapo Allaah anaichukia shirki na ukafiri ni vipi basi atayakadiria mambo hayo? Ndio, ameyaumba hayo kutokana na hekima na ili watu waweze kupambanuka:
مَّا كَانَ اللَّـهُ لِيَذَرَ الْمُؤْمِنِينَ عَلَىٰ مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُطْلِعَكُمْ عَلَى الْغَيْبِ
“Haiwi kwa Allaah kuwaacha waumini katika hali mliyo nayo mpaka ampambanue mbaya na mwema. Na haiwi kwa Allaah akufunulieni ya ghaibu.”[3]
Hatuwezi kumtofautisha mtiifu na mtenda dhambi isipokuwa kwa matendo. Matendo ndio yanayompambanua mwangamivu kutokana na mwenye furaha. Mambo hayasilihi isipokuwa kukipatikana vinyume vyake.
[1] Muslim (8).
[2]21:35
[3]3:179
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 206-207
- Imechapishwa: 29/03/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 206-207
Imechapishwa: 29/03/2025
https://firqatunnajia.com/189-ndio-maana-allaah-akaumba-shari/