Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
141 – Pepo na Moto vimeshaumbwa. Kamwe havitoteketea wala kumalizika.
MAELEZO
Miongoni mwa mambo yatayokuwepo siku ya Qiyaamah ni Pepo, ambayo ni makazi ya wenye kumcha Allaah, na Moto ni makazi ya watenda madhambi. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu Pepo:
أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ
“… imeandaliwa kwa wenye kumcha Allaah.”[1]
Amesema kuhusu Moto:
أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ
”… umeandaliwa kwa makafiri.”
Kwa hivyo ni makazi mawili yenye kubaki na yapo hivi sasa. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ
“… imeandaliwa kwa wenye kumcha Allaah.”[2]
أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ
”… umeandaliwa kwa makafiri.”[3]
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhm) amesema:
“Siku moja wakati tulipokuwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tulisikia kitu kinachoanguka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mnajua ni kitu gani?” Akasema: “Allaah na Mtume Wake ndio wajuzi zaidi.” Ndipo Mtume akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Hilo ni jiwe lililotupwa ndani ya Moto tangu miaka sabini iliyopita. Hivi sasa ndio limefikia mwisho wake.”[4]
Inafahamisha kuwa Moto tayari umekwishaumbwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu joto na baridi:
“Moto ulilalamika kwa Mola ukasema: “Ee Mola! Nalika kwa ndani.” Akaupa idhini ya kupumua mara mbili; pumzi ya kwanza wakati wa masika na pumzi ya pili wakati wa kipwa. Ndio lile joto kali mnalohisi na baridi kali mnayohisi.”[5]
Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Siku moja tulikuwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) safarini. Muadhini akataka kutoa adhaana ambapo akamwambia: “[Subiri kuwe kidogo na] baridi.” Kisha akataka tena kuadhini ambapo akamwambia: “[Subiri kuwe kidogo na] baridi.”Kisha akataka tena kuadhini ambapo akamwambia: “[Subiri kuwe kidogo na] baridi.” Mpaka kivuli kilipolingana na vilima ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Hakika ukali wa joto ni katika uvukizi wa Jahannam.”[6]
Vivyo hivyo muumini ndani ya kaburi hufunguliwa mlango wa Pepo, na kafiri hufunguliwa mlango wa Moto. Haya yanafahamisha kuwa tayari Pepo na Moto vipo hivi sasa. ´Aqiydah hii wameipinga wapotofu, wanadai kuwa vitaumbwa siku ya Qiyaamah.
[1]03:133
[2]03:133
[3]2:24
[4]Muslim (2844).
[5]al-Bukhaariy (537) na Muslim (617).
[6]al-Bukhaariy (629) na Muslim (616).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 204-205
- Imechapishwa: 29/03/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)