Miongoni mwa dalili za adhabu ya kaburi ni maneno ya Allaah (´Azza wa Jall) kuhusu watu wa Fir´awn:
النَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا ۖ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ
“Wanadhihirishiwa moto asubuhi na jioni, na Siku itakayosimama Saa [kutasemwa]: “Waingizeni watu wa Fir’awn katika adhabu kali kabisa!”[1]
Kuonyeshwa Moto asubuhi na jioni ni jambo linafanyika ndani ya kaburi.
وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا عَذَابًا دُونَ ذَٰلِكَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
“Na hakika wale waliodhulmu watapata adhabu nyingine isiyokuwa hiyo, lakini wengi wao hawajui.”[2]
Wanazuoni wamesema kuwa ni adhabu ya kaburi. Kuna maoni mengine yanayosema kuwa ni adhabu inayowapata duniani katika kuuliwa, kushikwa mateka, kulipa kodi na mfano wa hayo. Aayah inakusanya maana zote mbili. Vilevile amesema (Ta´ala):
وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنَ الْعَذَابِ الْأَدْنَىٰ دُونَ الْعَذَابِ الْأَكْبَرِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
“Na bila shaka Tutawaonjesha adhabu ndogo kabla ya adhabu kubwa huenda wakajirejea.”[3]
Adhabu ndogo ni adhabu ya ndani ya kaburi na adhabu kubwa ni adhabu ya siku ya Qiyaamah.
Kuhusu Sunnah, zipo Hadiyth nyingi mno zinazothibitisha adhabu ya kaburi. Miongoni mwazo ni kwamba Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipita karibu na makaburi mawili akasema:
“Hakika wawili hawa wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa jambo kubwa. Bila shaka, ni jambo kubwa. Ama mmoja wao alikuwa akieneza uvumi na mwingine alikuwa hajichungi na cheche za mkojo.”[4]
Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ جهنم و من عَذَابِ الْقَبْر ومِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ وَ مِنْ فتنة الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ
“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba ulinzi kutokamana na adabu ya Jahannam na kutokamana na adhabu ya kaburi, kutokamana na fitina ya uhai na kifo na kutokamana na fitina ya al-Masiyh ad-Dajjaal.”[5]
Kuna watu ambao wanaweza kushuhudia adhabu ya kaburi kwa ajili ya mawaidha na mazingatio. Haafidhw Ibn Rajab (Rahimahu Allaah) ametaja mambo ya ajabu katika kitabu chake “Ahwaal-ul-Qubuur” na kadhalika Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ametaja katika kitabu chake “ar-Ruuh” mambo ya ajabu. Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:
“… kutokana na vile ilivyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum).”
Kwa sababu neema na adhabu ya kaburi ni miongoni mwa mambo yaliyofichikana, mambo ambayo hayathibitishwi isipokuwa yale yaliyofahamishwa na dalili na hayakanushwi yale yaliyojulishwa na dalili. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
[1]40:46
[2]52:47
[3]32:21
[4]al-Bukhaariy (218) na Muslim (292).
[5]at-Tirmidhiy (3613) ambaye amesema ni nzuri na Swahiyh.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 196-198
- Imechapishwa: 11/12/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 196-198
Imechapishwa: 11/12/2024
https://firqatunnajia.com/181-dalili-ya-adhabu-ya-kaburi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)