Swali: Je, kuwasengenya watu kunafunguza katika Ramadhaan?
Jibu: Usengenyi hakumfunguzi mfungaji. Usengenyi maana yake ni kumsema nduguyo kwa kitu anachokichukia. Ni dhambi. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا
”Wala wasisengenyane baadhi yenu wengine.”[1]
Vivyo hivyo umbea, matusi, kulaani na wongo vyote hivo havimfunguzi mfungaji. Lakini hata hivo ni maasi ambayo ni lazima kwa mfungaji na mwengine kutahadhari na kujiepusha nayo. Ni madhambi ambayo yanaijeruhi na kupunguza ujira wa swawm. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule asiyeacha maneno ya uongo, kuyatendea kazi na ujinga, basi Allaah hana haja kwa yeye kuacha chakula na kinywaji chake.”
Ameipokea Imaam al-Bukhaariy katika ”as-Swahiyh” yake.
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Swawm ni kinga. Itapokuwa ni siku ya funga ya mmoja wenu, basi asizungumze maneno machafu wala asipige kelele. Mtu akimtukana au akamgombeza, basi amwambie: “Mimi nimefunga.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Zipo Hadiyth nyingi zilizo na maana kama hii.
[1] 49:12
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ashyaa´ laa tufsid-is-Swawm, uk. 14
- Imechapishwa: 03/04/2021
Swali: Je, kuwasengenya watu kunafunguza katika Ramadhaan?
Jibu: Usengenyi hakumfunguzi mfungaji. Usengenyi maana yake ni kumsema nduguyo kwa kitu anachokichukia. Ni dhambi. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا
”Wala wasisengenyane baadhi yenu wengine.”[1]
Vivyo hivyo umbea, matusi, kulaani na wongo vyote hivo havimfunguzi mfungaji. Lakini hata hivo ni maasi ambayo ni lazima kwa mfungaji na mwengine kutahadhari na kujiepusha nayo. Ni madhambi ambayo yanaijeruhi na kupunguza ujira wa swawm. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule asiyeacha maneno ya uongo, kuyatendea kazi na ujinga, basi Allaah hana haja kwa yeye kuacha chakula na kinywaji chake.”
Ameipokea Imaam al-Bukhaariy katika ”as-Swahiyh” yake.
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Swawm ni kinga. Itapokuwa ni siku ya funga ya mmoja wenu, basi asizungumze maneno machafu wala asipige kelele. Mtu akimtukana au akamgombeza, basi amwambie: “Mimi nimefunga.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Zipo Hadiyth nyingi zilizo na maana kama hii.
[1] 49:12
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ashyaa´ laa tufsid-is-Swawm, uk. 14
Imechapishwa: 03/04/2021
https://firqatunnajia.com/18-usengenyi-unafunguza/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)