18. Rukuu´ na Sujuud vinafahamisha kujisalimisha kwa Allaah

Rukuu´ ni kuudhalilisha mwili. Kwa hiyo waarabu walikataa kusujudu. Baadhi yao walijaribu hata kumpa kiapo cha utii kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) wasujudu pasi na kuhitaji kuinama. Kwa maana nyingine wasujudu bila ya kurukuu, hivo ndivo alivyofasiri Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) na wanazuoni wengine wakaguzi. Amesema Allaah (Ta´ala):

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لَا يَرْكَعُونَ

”Wanapoambiwa rukuuni, hawarukuu.”[1]

[1] 77:48

  • Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 74-75
  • Imechapishwa: 24/11/2025