18 – Ndio maana al-Madkhaliy alitaja matamko yote mawili kuhusu Wahdat-ul-Wujuud

“Umefanya vizuri uliponukuu radd yake kwa nadharia ya viumbe vyote ni Allaah katika tafsiri ya “al-Baqarah”. Katika hayo ni pamoja na maneno yake: “Kuanzia hapa nadharia ya viumbe vyote ni Allaah imeisha kutokamana na fikira ya Kiislamu sahihi.””

Ninamuomba Allaah anifanye niweze kufanya vizuri katika maneno na matendo yangu yote na pamoja vilevile na mjadala wangu na Sayyid Qutwub.

Lakini hata hivyo utambue kuwa sikuyataja maneno yake kwa ajili ya kumtetea. Kwa sababu hapo itakuwa na maana ya kuwaghushi waislamu. Nimeyataja ili kuwaraddi wale wenye kusema kuwa maneno haya yanapatikana katika chapa ya pili na hivyo yamefuta maneno yake katika “al-Hadiyd” na “al-Ikhlaasw” katika ile chapa ya kwanza. Nimeiraddi shubuha hii na kuonyesha kuwa mambo yalivyo ni kinyume na kwamba aliyoyasema katika tafsiri ya “al-Baqarah” yaliandikwa kabla ya nadharia ya kwamba viumbe wote ni Allaah katika tafsiri ya “al-Hadiyd” na “al-Ikhlaasw”. Kwa mujibu wa istilahi ya Qutbiyyuun na istilahi yenu tafsiri ya Qutwub katika “al-Hadiyd” na “al-Ikhlaasw” pamoja na yale aliyoashiria katika “al-Kawthar” yanafuta tafsiri yake katika “al-Baqarah”.

Nilikubainishieni katika “Adhwaa´ Islaamiyyah” kujigonga kwa watu wenye nadharia ya kwamba viumbe vyote ni Allaah, na khaswa khaswa Ibn ´Arabiy, hakukuwazuia wanachuoni kuwahukumu ya kwamba ni watu wenye nadharia hii na wenye nadharia ya kwamba Allaah amekita na kuchanganyika na viumbe vyote[1]. Ukipenda rejea katika maneno ya Shaykh-ul-Islaam:

“Ibn ´Arabiy ana I´tiqaad nne:

1- ´Aqiydah ya Abuul-Ma´aaliy na wafuasi wake isiyokuwa na hoja yoyote.

2- ´Aqiydah hiyo hiyo kwa hoja za kifalsafa

3- ´Aqiydah ya Ibn Siynaa na watu mfano wake ambao wanatofautisha kati ya wajibu na kitu chenye uwezekano kuwepo.

4- Uchunguzi aliyofikia, nao si mwengine ni kwamba kuna uwepo mmoja.”[2]

[1] Huluul.

[2] an-Nubuwwaat, uk. 119-120.