12 – Havui nguo zake katika isiyokuwa nyumba ya mume wake. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanamke yeyote atakayevua nguo zake katika nyumba isiyokuwa yake, basi Allaah ataivunja sitara kutoka kwake.”[1]
al-Munaawiy amesema:
“Allaah (´Azza wa Jall) atavunja sitara kutoka kwake kwa sababu wakati aliposhindwa kuhifadhi yale aliyoamrishwa kuyafunika kutokamana wanamme wa kando naye ndipo akalipwa kufanyiwa hivo – malipo yanatokana na mtu alivyotenda. Udhahiri ni kwamba kuvua nguo ni ibara kuhusu kujifunua mbele ya wanamme wa kando naye kwa ajili ya jimaa au vile vitangulizi vyake. Ni tofauti na pale anapovua nguo zake kati ya wanawake wenzake sambamba na kufunika vile viungo visivyotakiwa kuonekana. Katika hali hiyo hakuna nafasi na yeye kuingia katika matishio haya.”[2]
[1] al-Haakim (04/289) na wengineo. Inapatikana katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´ as-Swaghiyr” (2705).
[2] Fawdhw-ul-Qadiyr (03/147).
- Muhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 34-35
- Imechapishwa: 28/09/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)