6 – Upokezi wa Muhammad bin an-Nu´maan bin ´Abdis-Salaam at-Taymiy[1]
Abush-Shaykh al-Aswbahaaniy amesema: “´Abdur-Rahmaan bin al-Faydhw[2] ametuhadithia: Haaruun bin Sulaymaan[3] ametuhadithia: Nilimsikia Muhammad bin an-Nu´maan bin ´Abdis-Salaam akisema:
“Mtu mmoja alimjia Maalik bin Anas na kusema:
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[4]
Amelingana juu vipi?” Akainamisha kichwa na kuanza kutokwa na jasho. Tukangoja tuone nini atachoamrisha. Akainua kichwa chake na kusema: “Kulingana kutoka Kwake si kitu kisichotambulika, namna kutoka Kwake haifahamiki. Kuamini hilo ni wajibu na kuuliza juu yake ni Bid´ah. Mimi sikuoni vyengine isipokuwa mpotevu.” Mtoeni nyumbani kwangu.”[5]
Mlolongo wa wapokezi wake ni mzuri.
[1] Abu ´Abdillaah Muhammad bin an-Nu´maan bin ´Abdis-Salaam at-Taymiy al-Aswbahaaniy. Abush-Shaykh al-Answaariy amesema juu yake:
“Mwanachuoni wa Hadiyth, mwana wa mwanachuoni wa Hadiyth, mwana wa mwanachuoni wa Hadiyth. Alifariki mwaka 244. Amesimulia kutoka kwa Waky′, Ibn ´Uyaynah, Hafsw bin Ghiyaath, Abu Bakr bin Abiy ´Ayyaash na wengineo. Alikuwa mmoja katika wachaji Allaah, amesimulia Hadiyth chache na hakusimulia isipokuwa kiasi kidogo tu.” (Twabaqaat-ul-Muhaddithiyn bil-Aswbahaan (2/211))
adh-Dhahaby amesema juu yake:
“Shaykh wa Aswbahaan, mwana wa Shaykh wake na baba wa Shaykh wake. Abu ´Abdillaah.” (Taariykh-ul-Islaam, uk. 475, alifariki 241-250)
[2] Abul-Aswad ´Abdur-Rahmaan bin al-Faydhw bin Sandah bin Dhuhr. Mmoja katika watu madhubuti wa Aswbahaan. Tazama “Taariykh-ul-Islaam”, uk. 84, kafariki 321-330.
[3] Haaruun bin Sulaymaan al-Khazzaar al-Aswbahaaniy. Madhubuti. Alifariki ima mwaka wa 263 au 265. Tazama “Akhbaar Aswbahaan” (2/214) ya Abu Nu´aym.
[4] 20:05
[5] Twabaqaat-ul-Muhaddithiyn bil-Aswbahaan (2/214).
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 36-37
- Imechapishwa: 29/11/2025
6 – Upokezi wa Muhammad bin an-Nu´maan bin ´Abdis-Salaam at-Taymiy[1]
Abush-Shaykh al-Aswbahaaniy amesema: “´Abdur-Rahmaan bin al-Faydhw[2] ametuhadithia: Haaruun bin Sulaymaan[3] ametuhadithia: Nilimsikia Muhammad bin an-Nu´maan bin ´Abdis-Salaam akisema:
“Mtu mmoja alimjia Maalik bin Anas na kusema:
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[4]
Amelingana juu vipi?” Akainamisha kichwa na kuanza kutokwa na jasho. Tukangoja tuone nini atachoamrisha. Akainua kichwa chake na kusema: “Kulingana kutoka Kwake si kitu kisichotambulika, namna kutoka Kwake haifahamiki. Kuamini hilo ni wajibu na kuuliza juu yake ni Bid´ah. Mimi sikuoni vyengine isipokuwa mpotevu.” Mtoeni nyumbani kwangu.”[5]
Mlolongo wa wapokezi wake ni mzuri.
[1] Abu ´Abdillaah Muhammad bin an-Nu´maan bin ´Abdis-Salaam at-Taymiy al-Aswbahaaniy. Abush-Shaykh al-Answaariy amesema juu yake:
“Mwanachuoni wa Hadiyth, mwana wa mwanachuoni wa Hadiyth, mwana wa mwanachuoni wa Hadiyth. Alifariki mwaka 244. Amesimulia kutoka kwa Waky′, Ibn ´Uyaynah, Hafsw bin Ghiyaath, Abu Bakr bin Abiy ´Ayyaash na wengineo. Alikuwa mmoja katika wachaji Allaah, amesimulia Hadiyth chache na hakusimulia isipokuwa kiasi kidogo tu.” (Twabaqaat-ul-Muhaddithiyn bil-Aswbahaan (2/211))
adh-Dhahaby amesema juu yake:
“Shaykh wa Aswbahaan, mwana wa Shaykh wake na baba wa Shaykh wake. Abu ´Abdillaah.” (Taariykh-ul-Islaam, uk. 475, alifariki 241-250)
[2] Abul-Aswad ´Abdur-Rahmaan bin al-Faydhw bin Sandah bin Dhuhr. Mmoja katika watu madhubuti wa Aswbahaan. Tazama “Taariykh-ul-Islaam”, uk. 84, kafariki 321-330.
[3] Haaruun bin Sulaymaan al-Khazzaar al-Aswbahaaniy. Madhubuti. Alifariki ima mwaka wa 263 au 265. Tazama “Akhbaar Aswbahaan” (2/214) ya Abu Nu´aym.
[4] 20:05
[5] Twabaqaat-ul-Muhaddithiyn bil-Aswbahaan (2/214).
Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 36-37
Imechapishwa: 29/11/2025
https://firqatunnajia.com/18-masimulizi-ya-maalik-kwa-mujibu-wa-muhammad-at-taymiy/