73 – Abul-Hasan ´Abdur-Rahmaan bin Muhammad bin ´Ubaydillaah al-Aswbahaaniy ametukhabarisha nayo: Abul-Qaasim Sulaymaan bin Ahmad bin Ayyuub at-Twabaraaniy ametuhadithia: Ahmad bin Khaalid bin Yahyaa bin Hayyaan ar-Raqqiy ametuhadithia: Zuhayr bin ´Abbaad ametuhadithia: Abu Bakr ad-Daahiriy ´Abdullaah bin Hakiym ametuhadithia, kutoka kwa Ismaa´iyl bin Abiy Khaalid, kutoka kwa ash-Sha´biy, kutoka kwa al-Waliyd bin ´Uqbah, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kundi la watu wa Peponi watawaona kundi la watu wa Motoni waseme: ”Ni kipi kilichokuingizeni Motoni? Hakika si vyenginevyo kilichotufanya kuingia Peponi ni kwa ajili ya kukufunzeni.” Ndipo waseme: ”Tulikuwa tukikuamrisheni na hatutendi.”[1]

Sulaymaan amesema:

”Hakuna mwingine aliyesimulia kutoka kwa Abu Khaalid isipokuwa Abu Bakr ad-Daahiriy. Zuhayr amepwekeka katika kuisimulia.”

74 – Abul-Hasan ´Aliy bin Ahmad bin ´Umar bin Hafsw al-Muqriy ametukhabarisha: Abu ´Abdillaah Muhammad bin al-´Abbaas bin al-Fadhwl ametuhadithia huko Mosul: Muhammad bin Ahmad bin Abiyl-Muthannaa ametuhadithia: Muhaadhwir bin al-Muwarriy´ ametuhadithia: al-A´mash ametuhadithia, kutoka kwa Shaqiyq bin Salamah, ambaye amesema:

”Kulisemwa kuambiwa Usaamah bin Zayd: ”Si wende kwa ´Uthmaan na umzungumzishe?” Akasema: ”Nyinyi mnafikiri kuwa mimi simzungumzishi isipokuwa hadi nikusikilizisheni. Nimezungumza naye chemba pasi na kutaka kuanzisha jambo ambalo mimi ndiye wa kwanza kulianzisha. Simwambii mtu kuwa ndiye mbora wa watu hata kama atakuwa ni kiongozi wangu. Hakika mimi nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: ”Ataletwa mtu siku ya Qiyaamah na kuvugumizwa Motoni ambapo matumbo yake yatatoka nje.” Kutasemwa: ”Je, wewe sulikuwa ukiamrisha mema na ukikataza maovu?” Atasema: “Nilikuwa nikikuamrisheni mema lakini mimi mwenyewe siyafanyi na nikikukatazeni maovu lakini lakini mimi mwenyewe nayafanya.”

75 – Abu Sa´iyd Muhammad bin Muusa bin al-Fadhwl as-Swayrafiy ametukhabarisha: Abul-´Abbaas Muhammad bin Ya´quub al-Aswamm ametuhadithia: Yahyaa bin Abiy Twaalib ametuhadithia: ´Abdul-Wahhaab bin ´Atwaa’ ametukhabarisha: Abu Salamah ametukhabarisha, kutoka kwa Mansuur bin Zaadhaan, ambaye ameeleza:

”Nimezinduliwa kuwa kuna baadhi ya watu ambao watatupwa Motoni, wakazi wa Motoni wataudhiwa na harufu yao mbaya na waseme: ”Ole wako! Ulikuwa ukifanya nini? Haitoshi ile shari tuliyomo mpaka uje kutuadhibu na harufu yako ya mvundo?” Ndipo aseme: ”Mimi nilikuwa mwanachuoni, lakini sikunufaika na elimu yangu.”

76 – Abu Ja´far Muhammad bin Ja´far bin ´Allaan al-Warraaq amenikhabarisha: Abu ´Abdillaah al-Husayn bin Ahmad bin Muhammad bin as-Swaffaar al-Harawiy ametuzindua: Muhammad bin Ibraahiym al-Wakiyl ametukhabarisha: Muhammad bin Mahmuud as-Samarqandiy ametuhadithia: Nimemsikia – yaani Yahyaa bin Mu´aadh ar-Raaziy – akisema:

”Masikini yule ambaye elimu yake ni kwa hasara yake, ulimi wake ni mpinzani wake na uelewa wake unaondosha udhuru wake.”

77 – Kulisemwa wakiambiwa baadhi yao:

”Je, si utafute elimu?” Akajibu: ”Tayari nina wapinzani wengi katika elimu na hivyo sitaki kuwatafuta wengine.”

[1] Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu sana. Abul-´Aynaa´ amekiri kutunga na akasema mwenyewe:

”Mimi na al-Jaahidhw tulikuwa tukitunga Hadiyth kuhusu Fadak.”

ad-Daaraqutwniy amesema kuwa ”sio mwenye nguvu katika Hadiyth”. Jengine ni kwamba Ibn Jurayj na Abuz-Zubayr walikuwa wenye hadaa – na katika Hadiyth hii hakubainisha amesikia simulizi hiyo kutoka kwa nani.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 51-53
  • Imechapishwa: 12/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy