2 – Mapenzi
Miongoni mwa makosa yanayoenda kinyume na Shari´ah ni yale yaliyoenea kwa baadhi ya wasichana, khaswa wanafunzi wa kike, yale yanayoitwa kuwa ni mapenzi. Uhakika wa mambo ni kwamba jambo hili ni ugonjwa usiotibika. Isiweje hivo ilihali linapingana na Tawhiyd kwa vile yule mwenye kupenda anakuwa ni mwenye kushughulishwa na anayempenda. Anashughulishwa na kumtaja badala ya kumpenda Mola wake (Tabaarak wa Ta´ala). Kuna mwanamke mmoja katika wenye kupenda ambaye alimwandikia mpenzi yake akimwambia:
“Ninakukumbuka wewe nyakati zote, ninakukumbuka katika kurukuu kwangu, kusujudu kwangu na katika hali zote za swalah yangu.”
Namuomba Allaah usalama.
Utakuta moyo wa mwenye kupenda unateseka na yule anayempenda. Hakika anayependa kitu kwa kupitiliza mbali na Allaah basi ni lazima atateseka nacho. Mapenzi, ingawa mwenye nayo atapata ladha kwayo, basi ndio mateso makubwa ya moyo. Tunaona kuwa moyo wa mwenye kupenda unamuadhibu yeye utwevu lakini pasi na yeye kuhisi. Bali hakika mwenye kupenda anashughulishwa kutokana na manufaa ya dini na dunia yake.
Ee dada yangu muislamu! Mapenzi (العاشقة) ni kule kupitiliza katika kupenda kwa kiasi cha kwamba yule mpendwa anautawala moyo wa yule mwenye kupenda. Hali inafikia kwamba huyu mwenye kupenda hakosi kumtia akilini yule mpenzi wake, kumkumbuka, kumfikiria na hivyo kamwe hakosekani akilini mwake.
Kwa hivyo mche Allaah, ee msichana wa Kiislamu, na achana na jambo hili la khatari. Tambua ya kwamba dawa ya ugonjwa huu ni kuijua Tawhiyd ya Allaah, Sunnah, alama na utukufu Wake. Jengine zifanye zile ´ibaadah za nje na za ndani na ukithirishe kumrejea na kumnyenyekea Allaah ili akuondolee maradhi haya. Maradhi hayo hayana dawa inayonufaisha zaidi kuliko kumtakasia nia Allaah. Hiyo ndio dawa aliyoitaja ndani ya Kitabu Chake pale aliposema:
كَذَٰلِكَ لِنَصْرِفَ عَنْهُ السُّوءَ وَالْفَحْشَاءَ ۚ إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُخْلَصِينَ
”Tumefanya hayo ili Tumwepushe na uovu na machafu. Hakika yeye ni miongoni mwa Waja Wetu waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.”[1]
[1] 12:24
- Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 24-25
- Imechapishwa: 15/02/2026

Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 24-25
Imechapishwa: 15/02/2026
https://firqatunnajia.com/18-mapenzi-ya-kupitiliza/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket