Madhambi yanaiharibu akili. Hakika akili ina nuru. Maasi bila shaka yanaizima nuru ya akili. Pindi nuru yake inazimwa, hudhoofika na kupungua. Kuna baadhi ya Salaf wamesema:

“Hakuna yeyote anayemuasi Allaah isipokuwa mpaka kwanza akili yake itoweke.”

Huu ndio udhahiri wa mambo. Lau akili yake ingelikuwepo basi asingeliweza kumuasi Allaah ilihali yuko kwenye mikono ya Mola (Ta´ala), chini ya uendeshaji Wake, kwenye nyumba Yake na kwenye busati Yake. Malaika Wake wapo na ni wenye kumtazama. Mawaidha ya Qur-aan yanamkataza. Mawaidha ya imani yanamkataza. Mawaidha ya kifo yanamkataza. Mawaidha ya Moto yanamkataza. Kheri za duniani na Aakhirah anazokosa wakati anapotenda maasi ni nyingi kabisa kuliko ile furaha na ladha anayopata pindi anapotenda maasi. Hivi kuna yeyote aliye na akili iliyosalimika ambaye anatenda madhambi?

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 71-72
  • Imechapishwa: 08/01/2018