Tambueni ya kwamba ni wajibu kwa muislamu kutilia umuhimu dini yake na yale yanayoisahihisha, khaswa nguzo za Uislamu ambazo umejengwa juu yake. Miongoni mwao ni funga. Hii ni ´ibaadah Tukufu inayojirudia katika maisha ya muislamu mara moja tu kila mwaka.
Kwa sababu nguzo hizi tano za Uislamu, miongoni mwazo kuna ile inayomlazimu mja katika kila wakati wa maisha yake na ambayo haimwachi kamwe, nayo ni kuhushudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Miongoni mwazo kuna ile inayojirudia katika maisha ya muislamu kila siku na usiku mara tano, nayo ni swalah tano. Miongoni mwazo kuna ile inayojirudia kila mwaka, nayo ni zakaah na swawm. Miongoni mwazo kuna ile inayomlazimu muislamu mara moja tu katika umri wake, nayo ni Hajj iwapo atakuwa na uwezo wa kuiendea. Hivyo basi muislamu amefungamana na nguzo hizi kwa mafungamano makubwa na kujirudia kwake kila siku na kila mwaka ni kwa mujibu wa umuhimu wake na kwa namna ambayo anaweza kuzitekeleza bila mashaka.
Kisha nguzo hizi Tukufu miongoni mwazo kuna za kimwili tupu kama shahaadah, swalah na swawm, na miongoni mwazo kuna ya mali tupu nayo ni zakaah, na miongoni mwazo kuna ya kimwili na ya mali kwa pamoja ambayo ni Hajj. Ni lazima katika zote kuwepo nia mahsusi kwa ajili ya Allaah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakika si vyengineyo matendo yanategemea nia na kila mmoja atalipwa kutokana na vie alivyonuia.”[1]
Vilevile ni lazima zitekelezwe kwa namna iliyowekwa katika Shari´ah na inayoenda sambamba na yale yaliyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hadiyth inasema:
”Yeyote atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu, kitarudishwa.”[2]
Kwa hiyo ni wajibu kwa muislamu kuzitilia umuhimu nguzo za Uislamu na atekeleze kila nguzo kwa wakati wake uliopangwa hali ya kuwa ni mwenye kumtakasia nia Allaah na mwenye kwenda sambamba na Sunnah za Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] Muslim (1907).
[2] Muslim (1718), Ahmad (06/146).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 25
- Imechapishwa: 05/02/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 25
Imechapishwa: 05/02/2026
https://firqatunnajia.com/18-kutilia-umuhimu-dini-yako-na-khaswa-nguzo-za-uislamu/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket