Imamu wa maimamu Abu Bakr Muhammad bin Khuzaymah amesema:

”Mapokezi ya sifa yanaafikiana na Qur-aan. Vizazi vilivyokuja nyuma wameyapokea kutoka katika vile vizazi vilivyotangulia, kutoka kwa Maswahabah na wale waliokuja baada yao mpaka hii leo, kwa njia ya kwamba ni sifa za Allaah (Ta´ala). Mtu anatakiwa kuzitambua, kuziamini na kujisalimisha na yale Aliyoeleza (Ta´ala) katika wahy pamoja yale Nabii na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu Kitabu Chake. Mtu anatakiwa kufanya hivo pasi na tafsiri wala kukanusha, pasi na kushabihisha wala kufananisha.

Ibn Khuzaymah amekufa mwaka wa 311. Katika wakati wake hakukuwepo mtu mfano wake ambaye amekusanya kati ya Hadiyth na Fiqh. an-Naqqaash ameeleza ya kwamba amesema:

”Sijawahi kufata kipofo tangu nilipokuwa na miaka kumi na sita.”

Mwalimu wake al-Muzaniy amesema juu yake:

”Ni mjuzi zaidi wa Hadiyth kuliko mimi.”

93 – Abul-Hasan al-Ash´ariy amesema baada ya kutaja ´Aqiydah ya Khawaarij, Raafidhwah na Jahmiyyah:

“Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-ul-Hadiyth na Ahl-us-Sunnah. Miongoni mwa ´Aqiyah za Ahl-ul-Hadiyth was-Sunnah ni kumthibitisha Allaah, Malaika Wake, Mitume Yake, yote yaliyosemwa na Allaah na yale yote waliyoyapokea waaminifu kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawarudishi chochote katika hayo.

Wanathibitisha kuwa Allaah (Subhaanah) ni mungu Mmoja ambaye kila mmoja anamuhitaji na ambaye hamuhitaji yeyote. Hakuna mungu mwingine wa haki isipokuwa Yeye. Hakujifanyia mke wala mwana.

Wanathibitisha kuwa Muhammad ni mja na Mtume Wake, kwamba Pepo ni haki, kwamba Moto ni haki na kwamba Saa haina shaka yoyote kuwa itafika na kwamba Allaah atawafufua waliyomo ndani ya makaburi.

Wanathibitisha kuwa Allaah (Subhaanah) yuko juu ya ´Arshi Yake, kama Alivosema:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

Na kwamba yuko na mikono miwili isiyotakiwa kufanyiwa namna, kama Alivosema:

مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

”Kipi kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa mikono Yangu?”[2]

na:

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ

“Bali mikono Yake imekunjuliwa.”[3]

Na kwamba anayo macho mawili yasiyotakiwa kufanyiwa namna, kama Alivosema:

تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا

”Inatembea chini ya macho Yetu.”[4]

Na kwamba yuko na uso, kama Alivosema:

كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ

”Kila aliyekuwa humo [mbinguni na ardhini] atatoweka. Na utabakia uso wa Mola Wako wenye utukufu na wenye ukarimu.”[5][6]

Mwisho akasema:

”Yale yote niliyotaja juu yao ndio ´Aqiydah yangu ninayoamini.”

 Haya yametajwa na Imaam Abu Bakr bin Fawrak katika kitabu ”al-Khilaaf bayn Ibn Kullaab wal-Ash´ariy”. Kisha akasema mwishoni:

”Haya yanatilia mkazo juu ya kwamba ´Aqiydah ya Abul-Hasan al-Ash´ariy juu ya misingi hii ilikuwa misingi ya Ahl-ul-Hadiyth na misingi ya Tawhiyd.”

Abul-Hasan alikuwa anatambulika na hivyo hakuna haja ya kumtambulisha. Ukitaka kujua zaidi juu ya maisha yake, basi rejea katika kitabu cha ´Asaakir ”Tabyiynu Kadhib-il-Muftariy fiymaa nusiba ilaal-Ash´ariy”.

´Aqiydah hii al-Ash´ariy aliichukua kutoka kwa Zakariyyaa bin Yahyaa as-Saajiy, Shaykh wa Baswrah katika Hadiyth na Fiqh. Ameandika kitabu ”Ikhtilaaf-ul-Fuqahaa’” na ”´Ilal-ul-Hadiyth”. Alifariki mwaka wa 307.

[1] 20:5

[2] 38:75

[3] 5:64

[4] 54:14

[5] 55:26-27

[6] Maqaalaat-ul-Islaamiyyiyn (1/345).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 87-90
  • Imechapishwa: 04/06/2024