80 – Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: Ibn Abiy ´Adiy ametukhabarisha, kutoka kwa Salmaan, kutoka kwa Abu ´Uthmaan, kutoka kwa Usaamah bin Zayd, ambaye amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa akinishika mimi mkono wangu na mkono wa al-Hasan bin ´Aliy na akisema: ”Ee Allaah, wapende, kwani hakika mimi nawapenda!”[1]
81 – Sawwaar bin ´Abdillaah bin Sawwaar ametukhabarisha: al-Mu´tamir ametukhabarisha, kutoka kwa baba yake: Nimemsikia Abu Tamiymah akisimulia kutoka kwa Abu ´Uthmaan, kutoka kwa Usaamah bin Zayd, ambaye amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa akinichukua na kunikalisha juu ya paja lake na akimkalisha al-Hasan bin ´Aliy juu ya paja lake lingine, kisha akitutua chini na kusema: ”Ee Allaah, hakika mimi nawapenda, basi Nawe pia wapende!”[2]
82 – Haaruun bin Muusa ametukhabarisha: Muhammad bin Fulayh ametukhabarisha, kutoka kwa Muusa bin ´Uqbah, kutoka kwa az-Zuhriy: Saalim bin ´Abdillaah amesema: ´Abdullaah amesema:
”Watu walisema vibaya uongozi wa Usaamah bin Zayd, ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: ”Ikiwa mnasema vibaya uongozi wa Ibn Zayd, basi hapo kabla mlikuwa mkisema vibaya uongozi wa baba yake. Naapa kwa Allaah! Alikuwa anastahiki kwa uongozi na alikuwa ni miongoni mwa wale watu wanaopendeza zaidi kwangu. Baada yake huyu pia ni miongoni mwa watu wanaopendeza zaidi kwangu. Nakuusieni kumfanyia wema, kwani yeye ni miongoni mwa wabora wenu!”[3]
83 – ´Amr bin Yahyaa bin al-Haarith ametukhabarisha: al-Mu´aafaa ametukhabarisha: Zuhayr ametukhabarisha: Muusa bin ´Uqbah ametukhabarisha, kutoka kwa Saalim bin ´Abdillaah, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar, ambaye amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimteua Usaamah kuwa kiongozi na baada ya hapo akafikiwa na khabari kwamba watu wanamtia kasoro Usaamah na kuusema vibaya uongozi wake. Akasema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): “Hakika nyinyi mnamtia kasoro Usaamah na kuusema vibaya uongozi wake. Ndivyo mlivyofanya hapo awali na baba yake. Alikuwa anastahiki zaidi kwa uongozi na alikuwa ni miongoni mwa wale watu wanaopendeza zaidi kwangu. Hakika mwanawe huyu pia, baada yake, ni miongoni mwa watu wanaopendeza zaidi kwangu. Hivyo basi, nakuusieni kumfanyia wema, kwani yeye ni miongoni mwa wabora wenu!” Saalim amesema: “Sijawahi kumsikia ´Abdullaah bin ´Umar akisimulia Hadiyth hii isipokuwa pia alisema: “Isipokuwa kwa Faatwimah.”
[1] al-Bukhaariy (3747).
[2] al-Bukhaariy (3747).
[3] al-Bukhaariy (4250) na Muslim (2426).
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 70-71
- Imechapishwa: 09/09/2026

Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 70-71
Imechapishwa: 09/09/2026
https://firqatunnajia.com/18-fadhilah-za-usaamah-bin-zayd/