Lakini ikiwa atafungua kwa kula au kunywa kwa makusudi, basi amestahiki maonyo makali na hakika amefanya kosa kubwa. Hivyo inamlazimu kutubia, kujuta na kuomba msamaha. Aidha inamlazimu kulipa siku hiyo. Baadhi yao wamemlazimu kulipa pamoja na kutoa kafara. Hayo ndio madhehebu ya Maalik[1].
Ikiwa atafanya jimaa kwa makusudi, basi pia atakuwa amefanya kosa kubwa na inamlazimu kutubia na kuomba msamaha na kujuta na kulipa siku hiyo. Aidha inamlazimu kafara iliyo nzito nayo ambayo ni kuacha huru mtumwa, ikiwa hatapata basi afunge miezi miwili mfululizo, ikiwa hawezi basi alishe chakula masikini sitini, jambo ambalo ufafanuzi wake utakuja katika kisa cha bedui aliyefanya jimaa katika mchana wa Ramadhaan katika Hadiyth inayofuata. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakika si vyenginevyo Allaah ndiye kamlisha na kumnywesha.”
amehusisha kula na kunywa kwa Allaah, kwa sababu kusahau hakimilikiwi na mtu, bali Allaah ndiye anayemiliki kila kitu. Usahaulifu ni katika rehema ya Allaah kwa mja wake. Katika rehema Yake pia ni kuwa ameondosha dhiki kwa mja na hivyo amefanya kula na kunywa kwa kusahau hakuharibu ile swawm.
[1] Tazama ”at-Tafriy´ fiy Fiqh Imaam Maalik (01/175) na ”ar-Risaalah”, uk. 61 ya al-Qayrawaaniy.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Taysiyr Dhil-In´am bisharh ´Umdat-il-Ahkaam (01/446-447)
- Imechapishwa: 04/03/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)