al-Halabiy amesema:
“Kujigonga kwa Shaykh Rabiy´ hakukomekea hapo tu. Bali kumeenda mpaka katika kujielezea mwenyewe na juu ya maisha yake. Mfano wa hilo ni yale niliyoyathibitisha katika makala yangu “al-´Ibrah bi Nihaayat-ish-Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy as-Salafiyyah la bi Naqsw Bidaayatihi al-Ikhwaaniyyah al-Bid´iyyah”:
“Kujigonga kwa maneno ya Shaykh Rabiy´ ya mwanzo na ushahidi wa wanachuoni juu yake. Yeye mwenyewe amesema katika “Inqidhwaadhw-ush-Shuhub as-Salafiyyah”:
“Sijawahi kuwa Ikhwaaniy kamwe. Nilienda nao tu kwa muda kwa sharti wawatoe Ahl-ul-Bid´ah kutoka katika safu zao na kuwafunza vijana mfumo wa Salaf. Nilitangamana na watu wenye kujinasibisha na mfumo wa Salaf na si pamoja na Ahl-ul-Bid´ah wao. Hali kadhalika Salafiyyuun wengine walifanya hivi ikiwa ni pamoja na Shaykh al-Albaaniy. Je, unamaanisha, ´Adnaan, ya kwamba al-Albaaniy alikuwa ni Ikhwaaniy au ndani yake al-Ikhwaan? Je, unataka ajirejee?”
1- Ninazidi kukutilia mkazo wewe na watu mfano wako katika wafuasi wa al-Ikhwaan ya kwamba sijapatapo kuwa Ikhwaaniy. Nilikuwa dhidi ya njia zao za kisiasa. Nilikuwa nikiwanasihi kikweli na kuwalingania katika mfumo wa Salaf. Ni mara kidogo sana walikuwa wakitendea kazi usulubu wao wa kikweli mbele yangu. Walikuwa wanajua kuwa ningeliwakosoa na kuwakaripia kwa mwenendo wao. Sijawahi katu kulingania kitu katika mfumo wao. Ninaupiga vita na mfano wake katika durusi zangu. Mfumo wa Salaf daima ndio ilikuwa Da´wah yangu.
2- Shughuli yako kubwa umefanya ni kumpiga vita Rabiy´ wakati wewe umepiga mbizi kwenye upotevu na kuwatetea wapotevu waliovuka mipaka na upotevu wao. Matendo yako ni ya khatari sana kabisa.
3- Leta ushahidi wa wanachuoni waaminifu juu ya kujigonga kwa Rabiy´. Ninakusudia wanachuoni wa kweli kama Ibn Baaz, al-Albaaniy, Ibn ´Uthaymiyn, an-Najmiy, al-Fawzaan na al-Luhaydaan. Simaanishi Ahl-ul-Ahwaa´ wenye kulingania katika umoja wa dini na kuwatetea. Ikiwa hukuleta ushahidi huu basi wewe ni mwongo mtenda madhambi anapoteta na mwenye kufanana na Jahmiyyah wenye kuwatuhumu Ahl-us-Sunnah kuwa ni wenye kujigonga. Bali uhakika wa mambo ni kuwa matamanio yamewafanya kupinda mpaka kufikia kusema kuwa Qur-aan ni yenye kujigonga. Uongo wao umevunjwa-vunjwa na maimamu wa Uislamu na khaswa Imaam wa Ahl-us-Sunnah Ahmad bin Hanbal wakati alipoponda-ponda batili yao na kufichukua ujinga wao. Hali kadhalika akafanya Imaam ´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy. Jahmiyyah ndio wahenga wa al-Halabiy.
Himdi zote ni za Allaah sijapatapo kamwe kuwa Ikhwaaniy. Kama ulivyoninukuu mwenyewe ni kwamba nilikuwa pamoja nao kwa sharti wawafunze vijana mfumo wa Salaf na wazisafishe safu zao kwa kuwaondosha wapotevu. Kwa miaka mingi nilikuwa nao siku zote juu ya masharti haya. Niliwavumilia kidogo zaidi kuliko jinsi nilivyomvumilia al-Halabiy mwenda na watu. Kisha nikaachana nao kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall).
Ukinituhumu kujigonga basi unatakiwa ufanye vivyo hivyo na Shaykh al-Albaaniy ambaye alikuwa nao kwa muda mrefu ili kuwanyoosha. Hakuwaacha mpaka wao walipomwacha. Usipofanya hivo basi wewe ni katika watu wenye kujigonga vibaya sana. Una kujigonga kunakoangamiza kiasi gani!
Kujigonga huku kwa al-Halabiy ambaye anaenda na watu ni katika wafuasi wakubwa wa mfumo wa al-Khwaan al-Muslimuun na misingi yao. Miongoni mwa misingi hiyo ni pamoja na “mfumo mpana na wenye nafasi” wenye kuingiza Ahl-us-Sunnah na Ummah mzima. “Mfumo mpana” huu ameutumia kwa watu wanaolingania katika umoja wa dini, udugu wa dini na uhuru wa dini na kusapoti kampeni hizi. Bali amezidisha misingi inayoenda kinyume na mfumo wa Salaf ambayo hawana.
Nitataja vitabu vyangu ambapo nimewakemea al-Ikhwaan al-Muslimuun na viongozi wao. Vitabu hivyo vimewafichukua na watetezi wao kutoka katika pote la al-Halabiy. al-Halabiy anawasapoti pindi anapowatetea al-Ikhwaan al-Muslimuun na upotevu wao kama umoja wa dini, udugu wa dini na uhuru wa dini.
Rabiy´ bin Haadiy ´Umar al-Madkhaliy
1434-07-05
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
- Imechapishwa: 08/01/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
Imechapishwa: 08/01/2017
https://firqatunnajia.com/18-al-halabiy-anamtuhumu-rabiy-al-madkhaliy-kujigonga/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)