17. Zingatia, ee dada yangu muislamu!

Ee dada yangu muislamu! Ni ipi hali ya dada wa kiislamu ambaye yamemtokea hayo yaliyotangulia kusemwa au baadhi yake. Hakika anabakia hali ya kuwa ni mwenye huzuni na mwenye simanzi katika maisah yake yote, kwani ameuliwa pasi na kisu na amefikwa na kifo cha polepole. Mwanamke huyo anakuwa na khofu mumewe asije kujua. Kila ambapo mwanamke huyo anamuona mumewe akiwa ni mwenye huzuni, basi anajiambia mwenyewe kuwa amelijua jambo lake. Hali yake inakuwa namna hiyo pale asipokamatwa na mamlaka husika. Endapo atakamatwa basi jambo linakuwa baya na chungu zaidi.

Ee dada yangu muislamu! Lau ungelijua hali ya vijana wanaotumia mawasiliano mabaya ya simu kile wanachosema juu yako na watu mfano wako. Hakika hapana vyenginevyo wanatumia matamshi ambayo paji la uso linamwaga jasho kwa matamshi hayo iilihali eti wanafanya kukudhihirishia mapenzi na uaminifu, bali wanasimuliani baadhi kwa wengine yale mazungumzo na mahusiano yanayotokea baina yao. Lau kama sio kuogopa kuzijeruhi hisia na mazingatio mengine, ningesimulia baadhi ya matukio halisi ambayo paji la uso linamwaga jasho kwayo na moyo wa kila mwenye wivu unapata maumivu kwayo. Kwa hivyo pata mazingatio, ee dada yangu, na wala usidanganyike na watu waovu ambao wana ndimi mbili na kuyumbayumba kama mbweha.

Tambua, ee dada yangu, ya kwamba lengo la watu hawa ni kustarehe na mwanamke huyo kwa muda mfupi kisha wanashika njia na kuondoka na huku mwanamke huyo anabakia na aibu na maharibifu yake.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 12/02/2026

Turn on/off menu