Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba hakuna njia ya kumfikia Allaah (´Azza wa Jall) na kuingia Peponi isipokuwa kupitia ile njia aliyoiweka Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) kupitia kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Lau mfalme miongoni mwa wafalme atafungua mlango wa kuingia kwake na akatangaza kwamba anayetaka kumfikia basi aingie kupitia mlango ule. Mnasemaje juu ya wale wenye kwenda kuingia kwenye milango mingine? Je, watamfikia? Hapana, bila shaka. Mfalme mkubwa, Mfalme wa wafalme, Muumbaji wa viumbe amefanya njia ya kuelekea Kwake kwa yale waliyokuja nayo Mitume Wake na kwenye kilele chao ni wa mwisho wao Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye baada ya kutumilizwa kwake hawezi mtu yeyote kupata furaha isipokuwa kwa kufuata njia yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Uhakika wa mambo ni kwamba kumtukuza na kufanya adabu na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kufuata yale aliyofuata na kuacha yale aliyoacha. Kadhalika tusimtangulie mbele yake na tukasema katika dini yake yale ambayo hakusema au tukazua ndani ya dini yake yale ambayo hakuyaweka katika Shari´ah. Je, hivi kweli ni katika kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumtukuza mtu akazua katika dini yake kitu ambacho amesema juu yake:

“Kila Bid´ah ni upotevu”

“Mwenye kufanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[1]?

Je, huku kweli ni kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo ukaweka katika dini ya Allaah ambayo hakuyaweka?

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

“Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi. Hivyo atakupendeni Allaah na atakusameheni dhambi zenu na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[2]

[1] Muslim (1718).

[2] 03:31-32

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 05/08/2019