128 – Ibn Kaasib Ya´qub bin Humayd ametukhabarisha: Zakariyyaa bin Mandhur bin Tha´labah ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Haazim, kutoka kwa Sahl bin Sa´d, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mkononi Mwake! Lau kama dunia mbele ya Allaah ingelikuwa sawa na bawa la nzi, basi asingelimpa kafiri hata fumba ya maji.”[1]

129 – ´Uqbah bin Mukram ametukhabarisha: Yuunus bin Bukayr ametukhabarisha: Abu Ma´shar ametukhabarisha, kutoka kwa Sa´iyd al-Maqburiy, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Lau kama dunia mbele ya Allaah ingelikuwa na kheri sawa na bawa la nzi, basi asingelimpa kafiri hata fumba ya maji.”

130 – Ibraahiym bin al-Mustamirr al-´Uruuqiy: Abu Hammaam ametukhabarisha: Muhammad bin ´Ammaar al-Madiyniy ametukhabarisha: Nimemsikia Swaalih, mtumwa wa at-Taw-amah, akisema: Nimemsikia Abu Hurayrah akisimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Lau kama dunia mbele ya Allaah ingelikuwa sawa na bawa la nzi, basi asingelimpa kafiri hata fumba ya maji.”

[1] at-Tirmidhiy (2320), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni Swahiyh na ngeni. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (5292).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 01/07/2025