Tuzinduke ni namna gani tutafaidika na kufunga Ramadhaan katika kuhakikisha kumcha Allaah (Ta´ala). Kama tulivyotangulia kutaja mtu anajizuilia kutokana na yale mambo aliyoyazowea kwa ajili ya kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ni kwa nini basi asijizuilie kutokamana na yale mambo ya haramu ambayo Allaah amemuharamishia katika kila wakati na kila kipindi? Kuna mmoja katika Salaf ambaye aliulizwa kuhusu watu wanaomwabudu Allaah ndani ya Ramadhaan kwa njia ya kuhifadhi mambo ya faradhi na mambo ya wajibu. Lakini punde tu inapomalizika Ramadhaan wanayaacha na kuyapoteza mambo hayo kikamilifu. Wakasema:
“Ni uovu wa watu waliyoje ambao hawamtambui Allaah isipokuwa katika Ramadhaan peke yake.”[1]
Ni lazima kwa muislamu awe mwenye kumchunga Allaah na kuhifadhi kumtii Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ndani ya Ramadhaan na miezi mingine. Hii ndio maana ya maneno Yake:
يأيها الذينءامنوا كتب عليكم الصيام كما كتب على الذين من قبلكم لعلكم تتقون
“Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa kufunga kama ilivyofaradhishwa kwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allaah.”[2]
Bi maana ili muweze kupata kumcha Allaah kupitia mwezi huu mtukufu na kupitia kuhifadhi kwenu kumtii Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Kwa ajili hii Ramadhaan ikawa ni fursa kubwa na yenye thamani ili kuweze kujifanyia akiba ya kumcha Allaah. Allaah (Jalla wa ´Alaa) anasema:
وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ
“Chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu nikumcha Allaah.”[3]
إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ
”Hakika mbora zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni yule mwenye kumcha Allaah zaidi kati yenu.”[4]
Ni fursa yenye thamani katika mwezi huu mtukufu kujifanyia akiba ya kumcha Allaah na tutoke ndani ya masomo ya Ramadhaan hali ya kuwa ni wenye kumcha Allaah (Tabaarak wa Ta´ala), wenye kuzowea kuhifadhi kumtii Allaah na kutekeleza maamrisho Yake (Subhaanahu wa Ta´ala).
[1] Tazama ”Latwaaif-ul-Ma´aarif”, uk. 396.
[2] 01:183
[3] 02:197
[4] 49:13
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Wa jaa´ Shahru Ramadhwaan, uk. 26-28
- Imechapishwa: 18/04/2022

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Wa jaa´ Shahru Ramadhwaan, uk. 26-28
Imechapishwa: 18/04/2022
https://firqatunnajia.com/17-ramadhaan-fursa-kubwa-na-yenye-thamani/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket