5 – Miongoni mwa shubuha zao ni kutumia kwao dalili Hadiyth isemayo:
“Shaytwaan amekata tamaa ya kuabudiwa katika kisiwa cha kiarabu.”
Ni Hadiyth Swahiyh ambayo imepokelewa kupitia njia nyingi katika “as-Swahiyh” ya Muslim na nyenginezo. Imetumiwa kama dalili juu ya kutokuwezekana kabisa kutokea shirki katika bara arabu. Jibu juu ya hilo ni kwa yale aliyosema Ibn Rajab (Rahimahu Allaah):
“Kinachokusudiwa ni kwamba amekata tamaa ummah mzima kukusanyika katika shirki kubwa.”
Ibn Kathiyr vilevile ameashiria maana hii wakati alipokuwa akifasiri maneno Yake (Ta´ala):
الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن دِينِكُمْ
“Leo hii wamekata tamaa wale waliokufuru na dini yenu.”[1]
Isitoshe kwa mujibu wa Hadiyth iliyotajwa hapo juu ukataji tamaa wa shaytwaan ni kwa kudhani na kwa kufikiria kwake na si kwamba amefanya hivo kwa ujuzi, kwa sababu hajui ghaibu. Haya ni mambo yaliyofichikana na hakuna ayajuaye isipokuwa Allaah pekee. Dhana yake hii inakadhibishwa na Hadiyth zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambazo ameeleza ndani yake kwamba kutatokea shirki katika ummah huu baada yake na uhalisia wa mambo vilevile unamkadhibisha. Kwani waarabu wengi wameritadi kutoka katika Uislamu baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa aina mbalimbali za kuritadi. Allaah ndiye anajua zaidi.
[1] 05:05
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 29-30
- Imechapishwa: 28/03/2019
5 – Miongoni mwa shubuha zao ni kutumia kwao dalili Hadiyth isemayo:
“Shaytwaan amekata tamaa ya kuabudiwa katika kisiwa cha kiarabu.”
Ni Hadiyth Swahiyh ambayo imepokelewa kupitia njia nyingi katika “as-Swahiyh” ya Muslim na nyenginezo. Imetumiwa kama dalili juu ya kutokuwezekana kabisa kutokea shirki katika bara arabu. Jibu juu ya hilo ni kwa yale aliyosema Ibn Rajab (Rahimahu Allaah):
“Kinachokusudiwa ni kwamba amekata tamaa ummah mzima kukusanyika katika shirki kubwa.”
Ibn Kathiyr vilevile ameashiria maana hii wakati alipokuwa akifasiri maneno Yake (Ta´ala):
الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن دِينِكُمْ
“Leo hii wamekata tamaa wale waliokufuru na dini yenu.”[1]
Isitoshe kwa mujibu wa Hadiyth iliyotajwa hapo juu ukataji tamaa wa shaytwaan ni kwa kudhani na kwa kufikiria kwake na si kwamba amefanya hivo kwa ujuzi, kwa sababu hajui ghaibu. Haya ni mambo yaliyofichikana na hakuna ayajuaye isipokuwa Allaah pekee. Dhana yake hii inakadhibishwa na Hadiyth zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambazo ameeleza ndani yake kwamba kutatokea shirki katika ummah huu baada yake na uhalisia wa mambo vilevile unamkadhibisha. Kwani waarabu wengi wameritadi kutoka katika Uislamu baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa aina mbalimbali za kuritadi. Allaah ndiye anajua zaidi.
[1] 05:05
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 29-30
Imechapishwa: 28/03/2019
https://firqatunnajia.com/17-radd-juu-ya-utata-wa-kwamba-hakuwezi-kutokea-shirki-katika-kisiwa-cha-kiarabu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket