Mwanamke wa Kiislamu anamuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa kutimiza haki za mume wake zilizo juu yake. Anahesabu thawabu na mwisho mwema kutoka kwa Mola Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Hatimizi haki za mume wake kwa njia ya nipe nikupe; akimpa na yeye anampa na asipompa na yeye hampi. Anampa kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hamna jukumu zaidi ya yale yaliyowekwa juu yenu na wao wana jukumu tu kwa yale yaliyowekwa juu yao.”[1]
Anatimiza uwajibu wake kwa kuwa anajua kuwa Allaah (´Azza wa Jall) Hayaachi matendo mema yakaenda bure. Mwanamke mzuri wa Kiislamu anajua kuwa haki za mume wake ni kubwa katika Uislamu. Mtume wake mpendwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Lau ningelimwamrisha yeyoye kumsujudia mwengine basi ningelimwamrisha mwanamke amsujudie mume wake. Mwanamke anakuwa hajatimiza haki za mume wake mpaka pale ambapo atataka kufanya jimaa na yeye wakati amekaa juu ya saruji ndogo na akamuitikia.“[2]
Mtume mtukufu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanamke hatopata ladha ya imani mpaka atimize haki za mume wake.”[3]
Mwanamke wa Kiislamu hupata ladha ya imani pale anapotimiza haki za mume wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanamke hatimizi haki za Allaah mpaka pale atapotimiza haki za mume wake.”[4]
Mwanamke mwema kwa moyo wote anatimiza haki za mume wake. Hakifanyi chochote [kuonekana] kikubwa kwa yale anayomtekelezea mume wake. Kwa nini? Kwa kuwa anajua kuwa Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kwa njia iliokuwa kubwa pindi aliposema kuwa vovyote mwanamke atavyomfanyia mume wake bado mume wake atakuwa siku zote anastahiki bora zaidi ya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Lau ingelikuwa ni sawa kwa mtu kumsujudia mtu mwingne basi ningelimwamrisha mwanamke kumsujudia mume wake kutokamana na ukubwa wa haki zake juu yake.”[5]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema vilevile:
“Lau mwanamke kihakika angelijua ni haki gani mume wake yuko nazo kwake basi asingelikaa chini wakati kinapotengwa chakula chake cha mchana na cha usiku mpaka pale anapomaliza kula.”[6]
Wakati mwanamke mwema wa Kiislamu anapotimiza haki za mume wake hamkumbushi hilo. Hakika anatambua ni haki gani yuko nazo juu yake kwa sababu anatenda kwa mujibu wa dini yake na anazingatia maneno ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye Mola Wake amesema juu yake:
لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
“Kwa hakika amekujieni Mtume anayetokana na nyinyi wenyewe, ni magumu juu yake [yanamhuzunisha] yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni [kwa kukujalini], mwenye huruma mno kwa waumini, mwenye rehma.”[7]
Mwanamke mwema alobarikiwa anajua kuwa yeye sio mdoea kwenye nyumba yake. Anaijua ni nafasi ipi alonayo nyumbani kwake. Ni mchungaji wa nyumba yake na moja katika jukumu lake ni yeye kutimiza haki hii ya mume wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:Hajali mashambulizi ya mashetani wa kibinaadamu na wa kijini ambayo uinje wake ni rehema na wanazungumza juu ya haki za wanaadamu na undani wake ni adhabu ya wazi. Shetani anawatumia marafiki zake wa kibinaadamu na wa kijini ili waiharibu nyumba ya mwanamke.”
“Mwanamke ni mchungaji wa nyumba yake na ataulizwa kwa kile alichokichunga.”[8]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna mja yeyote ambaye Allaah Atamuwajibisha kuchunga wachunga wake na akafa katika hali fulani ambapo amefanya usaliti juu ya wachunga wake isipokuwa Allaah Atamharamishia juu yake Pepo.”[9]
Ni lazima kuwafunza wanawake yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya haki za mume ili mwanamke aweze kumridhisha Mola Wake na furaha ihakikishwe kwenye nyumba yake.
[1] Muslim (1846).
[2] at-Twabaraaniy (5/5116-5117). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (3366).
[3] al-Haakim (4/7325) ambaye amesema iko kwa masharti ya al-Bukhaariy och Musim och adh-Dhahabiy ameafikiana naye.
[4] at-Twabaraaniy (4/7325). Mnyororo ni mzuri kwa mujibu wa al-Mundhiriy katika ”at-Targhiyb” (3/2986). al-Haythamiy amesema: ”Wanaume wake ni wanaume Swahiyh mbali na al-Mughiyrah bin Muslim ambaye hata hivyo ni mwaminifu.” (Majma´-uz-Zawaaid (5/5084)). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (3366) na ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1942).
[5] Ahmad (3/158), al-Bazzaar (13/6452) na an-Nasaaiy (5/9147). Mnyororo ni mzuri kwa mujibu wa al-Mundhiriy katika ”at-Targhiyb” (3/35) ambaye amesema: ”Wapokezi wake ni waaminifu na wanajulikana.” Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy kutokana na mapokezi mengine katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1936). Tazama ”al-Irwaa’” (7/55).
[6] at-Twabaraaniy (20/333) na al-Bazzaar (7/2665).
[7] 09:128
[8] al-Bukhaariy (893) na Muslim (1829).
[9] Muslim (142).
- Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 26-29
- Imechapishwa: 24/03/2017
Mwanamke wa Kiislamu anamuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa kutimiza haki za mume wake zilizo juu yake. Anahesabu thawabu na mwisho mwema kutoka kwa Mola Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Hatimizi haki za mume wake kwa njia ya nipe nikupe; akimpa na yeye anampa na asipompa na yeye hampi. Anampa kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hamna jukumu zaidi ya yale yaliyowekwa juu yenu na wao wana jukumu tu kwa yale yaliyowekwa juu yao.”[1]
Anatimiza uwajibu wake kwa kuwa anajua kuwa Allaah (´Azza wa Jall) Hayaachi matendo mema yakaenda bure. Mwanamke mzuri wa Kiislamu anajua kuwa haki za mume wake ni kubwa katika Uislamu. Mtume wake mpendwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Lau ningelimwamrisha yeyoye kumsujudia mwengine basi ningelimwamrisha mwanamke amsujudie mume wake. Mwanamke anakuwa hajatimiza haki za mume wake mpaka pale ambapo atataka kufanya jimaa na yeye wakati amekaa juu ya saruji ndogo na akamuitikia.”[2]
Mtume mtukufu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanamke hatopata ladha ya imani mpaka atimize haki za mume wake.”[3]
Mwanamke wa Kiislamu hupata ladha ya imani pale anapotimiza haki za mume wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanamke hatimizi haki za Allaah mpaka pale atapotimiza haki za mume wake.”[4]
Mwanamke mwema kwa moyo wote anatimiza haki za mume wake. Hakifanyi chochote [kuonekana] kikubwa kwa yale anayomtekelezea mume wake. Kwa nini? Kwa kuwa anajua kuwa Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kwa njia iliokuwa kubwa pindi aliposema kuwa vovyote mwanamke atavyomfanyia mume wake bado mume wake atakuwa siku zote anastahiki bora zaidi ya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Lau ingelikuwa ni sawa kwa mtu kumsujudia mtu mwingne basi ningelimwamrisha mwanamke kumsujudia mume wake kutokamana na ukubwa wa haki zake juu yake.”[5]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema vilevile:
“Lau mwanamke kihakika angelijua ni haki gani mume wake yuko nazo kwake basi asingelikaa chini wakati kinapotengwa chakula chake cha mchana na cha usiku mpaka pale anapomaliza kula.”[6]
Wakati mwanamke mwema wa Kiislamu anapotimiza haki za mume wake hamkumbushi hilo. Hakika anatambua ni haki gani yuko nazo juu yake kwa sababu anatenda kwa mujibu wa dini yake na anazingatia maneno ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye Mola Wake amesema juu yake:
لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
“Kwa hakika amekujieni Mtume anayetokana na nyinyi wenyewe, ni magumu juu yake [yanamhuzunisha] yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni [kwa kukujalini], mwenye huruma mno kwa waumini, mwenye rehma.”[7]
Mwanamke mwema alobarikiwa anajua kuwa yeye sio mdoea kwenye nyumba yake. Anaijua ni nafasi ipi alonayo nyumbani kwake. Ni mchungaji wa nyumba yake na moja katika jukumu lake ni yeye kutimiza haki hii ya mume wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:Hajali mashambulizi ya mashetani wa kibinaadamu na wa kijini ambayo uinje wake ni rehema na wanazungumza juu ya haki za wanaadamu na undani wake ni adhabu ya wazi. Shetani anawatumia marafiki zake wa kibinaadamu na wa kijini ili waiharibu nyumba ya mwanamke.”
“Mwanamke ni mchungaji wa nyumba yake na ataulizwa kwa kile alichokichunga.”[8]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna mja yeyote ambaye Allaah Atamuwajibisha kuchunga wachunga wake na akafa katika hali fulani ambapo amefanya usaliti juu ya wachunga wake isipokuwa Allaah Atamharamishia juu yake Pepo.”[9]
Ni lazima kuwafunza wanawake yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya haki za mume ili mwanamke aweze kumridhisha Mola Wake na furaha ihakikishwe kwenye nyumba yake.
[1] Muslim (1846).
[2] at-Twabaraaniy (5/5116-5117). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (3366).
[3] al-Haakim (4/7325) ambaye amesema iko kwa masharti ya al-Bukhaariy och Musim och adh-Dhahabiy ameafikiana naye.
[4] at-Twabaraaniy (4/7325). Mnyororo ni mzuri kwa mujibu wa al-Mundhiriy katika ”at-Targhiyb” (3/2986). al-Haythamiy amesema: ”Wanaume wake ni wanaume Swahiyh mbali na al-Mughiyrah bin Muslim ambaye hata hivyo ni mwaminifu.” (Majma´-uz-Zawaaid (5/5084)). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (3366) na ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1942).
[5] Ahmad (3/158), al-Bazzaar (13/6452) na an-Nasaaiy (5/9147). Mnyororo ni mzuri kwa mujibu wa al-Mundhiriy katika ”at-Targhiyb” (3/35) ambaye amesema: ”Wapokezi wake ni waaminifu na wanajulikana.” Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy kutokana na mapokezi mengine katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1936). Tazama ”al-Irwaa’” (7/55).
[6] at-Twabaraaniy (20/333) na al-Bazzaar (7/2665).
[7] 09:128
[8] al-Bukhaariy (893) na Muslim (1829).
[9] Muslim (142).
Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 26-29
Imechapishwa: 24/03/2017
https://firqatunnajia.com/17-ndio-maana-mwanamke-anatakiwa-kutimiza-haki-za-mume/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)