Kuhusu mtu aliyefanya jimaa katika mchana wa Ramadhaan hali ya kuwa amesahau, wanazuoni wamelkhitilafiana kuhusu yale yanayomlazimu. Je atalipa tu au analazimika pia kutoa kafara? Kuna maono mawili:

1 – Aliyesahau hawezi kupewa udhuru kwa kufanya jimaa katika mchana wa Ramadhaan. Kama ambavyo hapewi udhuru mwenye kufanya jimaa katika hajj, vivyo hivyo hawezi kupewa udhuru katika mchana wa Ramadhaan hata ikiwa amesahau. Haya ni madhehebu ya Maalikiyyah[1] na Hanaabilah[2] (Rahimahumu Allaah).

2 – Aliyesahau anapewa udhuru hata ikiwa katika jimaa. Dalili ya hilo ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Mwenye kufungua hali ya kuwa amesahau basi hakuna juu yake funga ya kulipa wala kafara.”[3]

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Mwenye kufungua… ”

yanajumuisha kula, kunywa na jimaa. Kwa hivyo hakuna juu yake funga ya kulipa. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”… wala kafara.”

kunamaanishwa jimaa, kwa sababu kafara ni maalum kwa jimaa. Kwa hiyo ni dalili ya kuwa ikiwa atafanya jimaa hali ya kuwa amesahau, basi swawm yake ni sahihi.

Haya ya pili ndio maoni sahihi kati ya maono miwili za wanazuoni. Ndio maoni ya Hanafiyyah[4] na Shaafi’iyyah[5]. Pia yamesemwa na Mujaahid na al-Hasan[6]. Aidha ath-Thawriy na Ishaaq[7] wameonelea hivo. Isitoshe ndio maoni ya wanazuoni wengi[8].

[1] Tazama “al-Mudawaanah  (01/277) na ”al-Kaafiy fiy Fiqhi Ahl-il-Madiynah” (01/341).

[2] Tazama ”al-Irshaad ilaa Sabiyl-il-Rashaad, uk. 146) na ”al-Mughniy (3/134) cha Ibn Qudaamah.

[3] Sunan ya al-Daaraqutwniy (2243), ”Sunan al-Kubraa” cha Al-Bayhaqiy (8074). Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Khuzaymah (1990), Ibn Hibbaan (3521) na al-Haakim (1569).

[4] Tazama ”al-Uswl-ul-Ma´ruuf bil-Mabsuutw” (02/201)  ya ash-Shaybaaniy  na ”al-Binaayah Sharh-il-Hidaayah (04/35).

[5] Tazama ”at-Tanbiyh fiy al-Fiqh-is-Shaafi’iy, uk. 66 na ”al-Bayaan fiy Madhhab al-Imaam al-Shaafi’iy (03/509).

[6] Swahiy-ul-Bukhaariy (01/31).

[7] Tazama ”Bidaayat-ul-Mujtahid (06/262), ”Sharh-us-Sunnah” (06/296) cha al-Baghawi na ”al-Binaayah Sharh-il-Hidaayah (04/35).

[8] Sharh an-Nawawiy ´alaa Muslim (08/35).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr Dhil-In´am bisharh ´Umdat-il-Ahkaam (01/444-446)
  • Imechapishwa: 03/03/2025