Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kitu cha kwanza Allaah alichoumba ni kalamu. Akaiambia: “Andika.” Ikasema: “Ee Mola! Niandike nini?” Akasema: “Andika makadirio ya kila kitu mpaka siku ya Qiyaamah.”[1]
Allaah aliiamrisha kalamu kuandika ambapo ikaandika kila kitu mpaka siku ya Qiyaamah. Fir´awn alimwambia Muusa:
قَالَ فَمَا بَالُ الْقُرُونِ الْأُولَىٰ قَالَ عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي فِي كِتَابٍ ۖ لَّا يَضِلُّ رَبِّي وَلَا يَنسَى
“Vipi kuhusu hali ya karne za mwanzo?” Akasema: “Ujuzi wake [kuhusu yaliyopitika] uko kwa Mola wangu [yameandikwa] katika Kitabu; hapotezi Mola wangu na wala hasahau.”[2]
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hakukosea na wala hasahau kitu. Hata hivyo katika hekima na njia Yake ni kuandika kila kitu. Vinginevyo hakuna haja ya kuandika kwa sababu hakukosea na wala hasahau. Katika uola Wake (Subhanaahu wa Ta´ala) ni kuwa Yeye anafanya kile Anachokitaka. Ameandika mambo yote haya aliyoyakadiria na akayaandika kwenye ubao Uliohifadhiwa. Ni ngazi ya kwanza ya Qadar; elimu na kuandika Kwake. Allaah daima alikuwa na ujuzi juu ya haraka, utulivu, makadirio, muda wa kueshi, urefu, ufupi, utajiri, ufakiri wa viumbe na vingine vyote. Kisha baada ya hapo akayaandika hayo yote kwenye ubao Uliohifadhiwa.
Ngazi zingine zote ni zenye kufuata ngazi hii ya kwanza. Nyingine ni kuandika. Makadirio ya kipomoko yanaandikwa pindi kinapopuliziwa roho. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anamwamrisha Malaika kuandika riziki yake, muda wake wa kueshi, matendo yake na kama atakuwa ni mla khasara au mwenye furaha. Uandishi huu ni wenye kufuata ule uandishi wa kwanza ambao unafuata ngazi ya elimu.
[1] Ahmad (5/317), Abu Daawuud (4700) na at-Tirmidhiy (2155). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (1/48).
[2] 20:51-52
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 28-29
- Imechapishwa: 15/10/2016
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kitu cha kwanza Allaah alichoumba ni kalamu. Akaiambia: “Andika.” Ikasema: “Ee Mola! Niandike nini?” Akasema: “Andika makadirio ya kila kitu mpaka siku ya Qiyaamah.”[1]
Allaah aliiamrisha kalamu kuandika ambapo ikaandika kila kitu mpaka siku ya Qiyaamah. Fir´awn alimwambia Muusa:
قَالَ فَمَا بَالُ الْقُرُونِ الْأُولَىٰ قَالَ عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي فِي كِتَابٍ ۖ لَّا يَضِلُّ رَبِّي وَلَا يَنسَى
“Vipi kuhusu hali ya karne za mwanzo?” Akasema: “Ujuzi wake [kuhusu yaliyopitika] uko kwa Mola wangu [yameandikwa] katika Kitabu; hapotezi Mola wangu na wala hasahau.”[2]
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hakukosea na wala hasahau kitu. Hata hivyo katika hekima na njia Yake ni kuandika kila kitu. Vinginevyo hakuna haja ya kuandika kwa sababu hakukosea na wala hasahau. Katika uola Wake (Subhanaahu wa Ta´ala) ni kuwa Yeye anafanya kile Anachokitaka. Ameandika mambo yote haya aliyoyakadiria na akayaandika kwenye ubao Uliohifadhiwa. Ni ngazi ya kwanza ya Qadar; elimu na kuandika Kwake. Allaah daima alikuwa na ujuzi juu ya haraka, utulivu, makadirio, muda wa kueshi, urefu, ufupi, utajiri, ufakiri wa viumbe na vingine vyote. Kisha baada ya hapo akayaandika hayo yote kwenye ubao Uliohifadhiwa.
Ngazi zingine zote ni zenye kufuata ngazi hii ya kwanza. Nyingine ni kuandika. Makadirio ya kipomoko yanaandikwa pindi kinapopuliziwa roho. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anamwamrisha Malaika kuandika riziki yake, muda wake wa kueshi, matendo yake na kama atakuwa ni mla khasara au mwenye furaha. Uandishi huu ni wenye kufuata ule uandishi wa kwanza ambao unafuata ngazi ya elimu.
[1] Ahmad (5/317), Abu Daawuud (4700) na at-Tirmidhiy (2155). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (1/48).
[2] 20:51-52
Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 28-29
Imechapishwa: 15/10/2016
https://firqatunnajia.com/17-makadirio-yameandikwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)