17. Maji yameingia tumboni mwake alipokuwa anaoga

Swali: Kuna mfungaji alioga na kwa sababu ya nguvu kubwa ya maji yakaingia tumboni mwake pasi na kutaka kwake. Je, analazimika kulipa?

Jibu: Halazimiki kulipa kwa sababu hakukusudia kufanya hivo. Huyu ana hukumu moja kama mwenye kutenzwa nguvu na mwenye kusahau.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ashyaa´ laa tufsid-is-Swawm, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 03/04/2021