92 – Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba inatakiwa kwa mja siku zote awe na woga muda yumo katika dunia hii, kwa sababu hajui atakufa katika hali gani, atahitimisha kwa kitu gani na atakutana na Allaah (´Azza wa Jall) na jipi, hata kama atafanya matendo yote ya kheri.
93 – Inatakikana kwa mtu mwenye kuifanyia israfu nafsi yake kutokata matumaini yake kwa Allaah (Ta´ala) wakati wa kufa, anatakiwa kumjengea dhana nzuri Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) na akhofu juu ya dhambi zake. Endapo Allaah atamrehemu, inatokamana na fadhilah Zake, na endapo Atamuadhibu, inatokamana na dhambi Zake.
94 – Inatakiwa kuamini ya kwamba Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) alimfanya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuyajua yatayowatokea ummah wake mpaka siku ya Qiyaamah.
95- Tambua ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ummah wangu utafarikiana katika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakasema: “Ni kina nani hao, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni wale wataokuwemo katika yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu.”[1]
Kwa maana ya Mkusanyiko.
Dini ilikuwa katika hali hii mpaka katika ukhalifah wa ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh). Hali kadhalika ndivyo hali ilivyokuwa katika zama za ´Uthmaan. Pindi alipouawa ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) ndipo kukaja tofauti na Bid´ah. Watu wakawa mapote na makundi. Hata hivyo kuna watu waliokuwa imara katika haki katika kile kipindi cha kwanza cha mabadiliko; wakazungumza kwayo, wakaitendea kazi na wakawalingania watu kwayo. Hali ikaendelea kuwa nzuri mpaka ilipofika tabaka la nne katika ukhalifah wa watu fulani. Ndipo zama zikabadilika, watu wakabadilika sana, Bid´ah zikaenea na wakakithiri walinganizi wanaolingania katika isiyokuwa njia ya haki na Mkusanyiko na kukapatikana mitihani katika kila jambo ambalo hakulizungumzia si Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah zake. Wakalingania katika mfarakano – ilihali Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza mfarakano – na baadhi wakawakafirisha wengine. Kila mmoja akawa analingania katika maoni yake na huku anamkufurisha yule mwenye kwenda kinyme naye. Matokeo yake wajinga, watu wa kawaida na watu wasiokuwa na elimu wakapotea. Wakawatamanisha watu na mambo ya kilimwengu na wakawatishia na adhabu za dunia. Hivyo watu wakawafuata kwa kuogopa juu ya dunia yao na kwa ajili ya kuipenda dunia yao. Sunnah na watu wake wakawa ni wenye kujificha. Bid´ah ikadhihiri na kuenea. Wakakufuru pasi na kujua kwa njia mbalimbali. Wakatendea kazi kipimo. Wakafasiri uwezo wa Allaah, Aayah, hukumu, maamrisho na makatazo Yake kwa mujibu wa akili na mitazamo yao. Yale yenye kuafikiana na akili zao wakakubalinaa nayo na yale yasiyoafikiana na akili zao wakayarudisha. Uislamu ukawa mgeni, Sunnah ikawa ngeni na Ahl-us-Sunnah wakawa ni wageni majumbani mwao.
[1] at-Tirmidhiy (2779) na al-Haakim (01/129).
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 96-98
- Imechapishwa: 22/12/2024

Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 96-98
Imechapishwa: 22/12/2024
https://firqatunnajia.com/17-kuwa-na-woga-daima/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)