Laiti madhara ya tofauti zao yangelibaki baina yao pekee na yasingelienea kati ya waislamu. Katika hali hiyo ingelikuwa jepesi kidogo. Tatizo ni kwamba madhara yake yameenea mpaka katika nchi na mabara ya kikafiri. Matokeo yake jambo hilo likawazuia wao kuingia katika dini ya Uislamu makundi kwa makundi. Muhammad al-Ghazaaliy amesema:

“Wakati wa mkutano uliofanyika katika chuo kikuu cha Princeton, Marekani, kuna mzungumzaji mmoja aliuliza swali lifuatalo:

“Ni Uislamu gani ambao waislamu wanatakiwa kujipamba nao ulimwenguni? Hebu watueleza ni Uislamu upi wanaoita kwao. Ni mafunzo ya Uislamu kwa mujibu wa uelewa wa wachina? Au ni mafunzo ya Uislamu, kwa mujibu wa uelewa wa Shiy´ah, kama mfano wa Imaamiyyah na Zaydiyyah? Jengine ni kwamba watu hawa wenyewe kwa wenyewe ni wenye kutofautiana. Baadhi yao wanaweza kufikiria mambo fulani kwa njia ya kisasa, ilihali wengine wanafikiria mambo hayo kwa njia ya kizamani. Kwa ufupi ni kwamba wale wanaolingania katika Uislamu wanawafanya wale walinganiwa ni wenye kudangana kama ambavyo wao wenyewe wamedangana.”[1]

[1] Dhwalaam-ul-Gharb, uk. 200

Mwishoni mwa uhai wake kitabu cha Muhammad al-Ghazaaliy kimeyafichua mambo mengi, kama mfano wa kilivofanya kitabu chake kwa kichwa cha khabari ”as-Sunnah an-Nabawiyyah bayn Ahl-il-Fiqh wa Ahl-il-Hadiyth”, na kwamba yeye mwenyewe ni katika mkumbo wa hao walinganizi waliodangana. Kupitia majibizano yangu mimi na yeye na kupitia vitabu vyake niliona mwenyewe kudangana kwake na kupondoka kwake kutokamana na Sunnah. Inapokuja katika kuzipa daraja Hadiyth, basi anategemea akili yake mwenyewe na wala sio katika vile vidhibiti vilivowekwa na wanachuoni. Ile Hadiyth inayompendeza, basi anaisahihisha japokuwa itakuwa ni dhaifu, na ile Hadiyth isiyompendeza, basi anaidhoofisha japokuwa itakuwa ni Swahiyh na iko kwa al-Bukhaariy na Muslim. Hayo uyatapata waziwazi katika Radd yake juu ya utangulizi wangu nilioandika wa chapa ya nne ya kitabu changu “Fiqh-us-Siyrah” . Yeye mwenyewe ndiye aliyeniomba kufanya hivo kupitia ndugu mmoja wa al-Azhar. Mara moja nikaanza kutaja vyanzo vya Hadiyth na kuzihukumu. Wakati huo nilikuwa nikidhani kuwa ni mtu anatilia umuhimu Sunnah na Siyrah ya kinabii na anapupia kutoingiza ndani yake vitu visivyotakikana. Hata kama alitangazia taaliki zangu na akazungumza kwa wazi juu ya kufurahishwa nazo, alieleza kuhusu mfumo wake wa kuzikubali Hadiyth zilizo dhaifu na kuzikataa Hadiyth zilizo Swahiyh na kwamba yeye hutazama matini ya ile Hadiyth peke yake. Hivyo hilo linampa hisia yule msomaji juu ya kwamba kazi hii ya kisomi haina uzito wowote kwake. Ukosoaji wake wa Hadiyth unatokana na nadharia peke yake. Ukosoaji kama huu unatofautiana kiasi kikubwa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine. Kile anachokikubali mtu kinakataliwa na mwingine na kinyume chake. Matokeo yake dini inakuwa ni matamanio yanayofuatwa na mtazamo wa mtu isiyokuwa na vidhibiti wala misingi. Hiki ni kitu kinachoenda kinyume na mfumo wa wanachuoni wote: cheni ya wapokezi ni katika dini; vinginevyo angelisema yeyote atakacho. Haya ndio yaleyale yaliyofanywa na al-Ghazaaliy juu ya Hadiyth nyingi katika ”Fiqh-us-Siyrah”. Kitabu chake kina kiwango kikubwa kabisa cha Hadiyth zilizo na cheni za wapokezi zilizokatika. Na zile zilizoungana zina udhaifu. Hayo atayaona kila yule ambaye atasoma taaliki zangu juu yacho. Pamoja na hivo anasema:

“Nimejitahidi kushikamana na mfumo bora na kutegemea marejeo yenye kuheshimiwa. Nafikiri kuwa nimefikia kiwango kizuri. Nimekusanya mapokezi mengi yanayompa yule mwanachuoni na mwenye uoni wa mbali utulivu wa nafsi.”

Lau angeulizwa ni kanuni zipi alizotumia mpaka kufikia katika Ijtihaad zake, basi asingelikuwa na jawabu yoyote isipokuwa kutegemea mtazamo wake mwenyewe. Mitazamo yake ina uharibifu tuliouashiria punde. Dalili ya hilo ni kwamba anasahihisha yale ambayo cheni ya wapokezi wake haikusihi na kuyadhoofisha yale ambayo cheni ya wapokezi wake imesihi hata kama ni katika al-Bukhaariy na Muslim. Hayo nimeyabainisha katika utangulizi wangu nilioashiria. Alivichapisha pamoja na toleo la nne la “Fiqh-is-Siyrah” kisha baadaye akayafuta katika toleo zilizofuatia baadaye, ikiwemo toleo lililotolewa na Daar-ul-Qalam Dameski. Jambo hilo liliwafanya watu kufikiria kwamba hakuomba kuandikiwa utangulizi isipokuwa tu kwa sababu aweze kukisambaza kitabu chake kati ya wasomaji wanaowaheshimu watu wanaoitumikia Sunnah, kuitetea na kupambanua kati ya Hadiyth ambazo ni Swahiyh na dhaifu kwa mujibu wa kanuni za kielimu na sio kwa mitazamo ya watu na matamanio yenye kutofautiana, tofauti na alivyofanya al-Ghazaaliy katika kitabu hiki na katika kitabu chake cha mwisho ”as-Sunnah an-Nabawiyyah bayn Ahl-il-Fiqh wa Ahl-il-Hadiyth”. Hivi sasa imewabainikia watu kuwa mfumo wake ni wa Mu´tazilah na kwamba anawapuuza na kuwadharau wanachuoni na juhudi zao kubwa za kuitumikia Sunnah. Kadhalika anawapuuza na kuwadharau wale maimamu na wanachuoni waliosimika misingi na kanuni na wakajenga mataga juu yake. Wanachuoni na watu waheshimiwa wengi wamemraddi. Allaah awajaze kila la kheri. Wamebainisha juu ya kudangana kwake na kupinda kwake. Miongoni mwa Ruduud nzuri nilizosoma ni ile iliyoandikwa na rafiki yetu Dr Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy na ikawekwa katika gazeti la kiafghani “al-Mujaahid” (nambari 09 na 11). Mwingine ni kitabu  ”al-Mi´yaar li ´Ilm al-Ghazaaliy” cha ndugu muheshimiwa Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz bin Muhammad Aalush-Shaykh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 59-61
  • Imechapishwa: 22/01/2019