Hata hivyo imethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba hakuna yeyote atakayemuona Allaah mpaka atakapokufa[1]. Wala hakuna dalili iliyothibiti inayojulisha kuwa yeye pia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona. Bali kumethibiti kinyume chake. Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Ee Mtume wa Allaah! Je, ulimuona Mola wako?” Akajibu: ”Ni Nuru. Nitamuonaje?”[2]

Isitoshe ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amelikanusha hilo[3], jambo ambalo ndio msingi na hivyo ndilo linalotakiwa kushikiliwa.

[1] Muslim.

[2] Muslim (178).

[3] al-Bukhaariy (4855) na Muslim (177).

  • Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 30
  • Imechapishwa: 18/09/2024