al-Halabiy amesema:
“Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy amesema: “Kuhusiana na wengine (Shu´bah, al-A´mash na wengine), nilinukuu maneno ya maimamu waadilifu juu ya kwamba walitumbukia kwenye Bid´ah ikiwa ni pamoja na madhehebu ya Qadariyyah, madhehebu ya Shiy´ah na madhehebu ya Murji-ah. Maimamu wa kujeruhi na kusifu wameyafikisha hayo katika vitabu vyao. Katika wasifu wa kila mmoja nimetaja Bid´ah na kila aliyetumbukia katika Bid´ah hizo na nikataja vyanzo. Maneno yangu ni ya kiuaminifu na hawawezi kuzingatia kuwa nimemtuhumu mtu kiungo.”
Ni pahali gani pa Kishari´ah kunaingia ukanushaji huu wa Shaykh Rabiy´ kwa kitu kilichothibiti kwake? Ninamwacha msomaji mwenye inswafu ajibu swali hili.”
1- Nimetazama vitabu vyangu juu ya yale ambayo al-Haddaad na al-Halabiy wameninasibishia pasi na kupata chochote. Na kama kweli mimi nimesema hivo, basi ninachomuabudu Allaah kwa kukiamini ni kwamba ninamzingatia Shu´bah na Suyfaan ath-Thawriy kuwa ni katika maimamu wa Uislamu ambao ninawapenda na kuwatukuza kwa ajili ya Allaah.
Kuhusiana na al-A´mash (Rahimahu Allaah), alitumbukia katika kitu katika Tashayyu´ lakini ambacho hakikumfanya akawachukia wala kuwasema vibaya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum).
Ama ambao mnaninasibishia kuwa nimesema kwamba wametumbukia katika madhehebu ya Qadariyyah na Murji-ah, nitajieni nao na mninukulie ili niweze kutamka msimamo wangu wa sawa juu yao.
2- Soma maneno aliyosema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):
“Wengi katika Mujtahiduun katika Salaf na waliokuja nyuma walifanya na kusema Bid´ah bila ya kujua kutokana na Hadiyth dhaifu ambazo walidhania kuwa ni Swahiyh, Aayah ambazo walizifahamu kimakosa au maoni yao katika mambo ambayo hawakujua dalili zake. Ikiwa mtu anamcha Allaah vile awezavyo basi anaingia katika Kauli Yake:
رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا |
“Mola wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea.” (02:286) |
Imepokelewa katika “as-Swahiyh” ya kwamba Allaah amesema:
“Nimefanya hivo.”[1]
3- Umeninukuu katika makala yako ya kwamba nimesema kuhusu Shu´bah:
“Shu´bah ni Imaam mkubwa na bali ni kiongozi wa waumini katika Hadiyth. Ametumia uhai wake katika kufunza na kusomesha Hadiyth na kuwachunguza wapokezi na alisafiri safari ndefu na za usumbufu kwa ajili ya Hadiyth moja.”[2]
Siku zote nimesema hivi na nitaendelea kusema hivo – Allaah akitaka – mpaka nitapokutana Naye.
4- al-Halabiy amesema:
Ni pahali gani pa Kishari´ah kunaingia ukanushaji huu wa Shaykh Rabiy´ kwa kitu kilichothibiti kwake? Ninamwacha msomaji mwenye inswafu ajibu swali hili.”
Ziko wapi dalili zako za wazi ambazo umejengea uthibitishaji huu juu yake?
Uzowefu wangu kwako ni kuwa unaeneza utata juu ya mapokezi ya kiuaminifu kiasi cha kwamba umefikia mpaka kueneza utata juu ya mapokezi ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), jambo ambalo linafanana na usulubu wa Raafidhwah.
Unasema kuwa unawapenda na kuwaheshimu Maswahabah pamoja na kuwa huonelei kuwa ni wenye kutukanwa wakati Sunniy anapowaita “povu” mpaka kuthibiti makubaliano ya kwamba ni tusi. Je, kuna upumbavu na mgongano wenye kutia aibu kushinda huu? Hakuna kimechokufanya kutumbukia kwenye mgongano huu isipokuwa ni matamanio, ushabiki wa kiupofu kwa yule aliyewatukana, mapenzi ya kupitiliza na kumtetea kwa batili.
Hukubali Tabdiy´ ya wanachuoni kwa mtu wa Bid´ah mpaka kuwepo makubaliano juu ya Tabdiy´ hiyo. Hili ni katika misingi yako iloharibika. Sambamba na hilo unakubali maneno ya watu wenye kwenda kinyume na mfumo wa Salaf ambayo baadae unajengea juu yake hukumu yako yenye kugonga. Je, kuna msingi na mgongano ulio mbaya zaidi kuliko huu?
Unajinasibisha na Salafiyyah wakati unatetea gazeti lililo na umoja wa dini, udugu wa dini na uhuru wa dini, ushuhuda wako wa uongo unaposema ya kwamba gazeti hilo limeupambanua Uislamu na kusema kuwa mamia ya watu wapotevu katika Raafidhwah, Khawaarij, Suufiyyah na wengine wenye kulisapoti ya kwamba ni wanachuoni waaminifu na viongozi waaminifu.
Unapenda na kuchukia kwa ajili ya mtu ambaye wazi wazi analingania katika umoja wa dini na unaenda bega kwa bega na watu wenye kulingania katika umoja wa dini na udugu wa dini.
Misimamo yako hii inauvunja Uislamu na Shari´ah kuanzia misingi yake na hujatubu kwa hali yoyote. Pamoja na yote haya wewe na watu mfano wako mnasema kuwa ni Salafiyyuun. Je, kuna mgongano ulio mbaya kabisa na mchafu kushinda huu? Halafu unasema kuwa wengine ndio wenye kujigonga. Mwenye kupeleleza vitabu vyako basi atakuja kuona kuwa wewe ni katika watu wenye kujigonga vibaya sana – mgongano uliojengwa juu ya ujinga na matamanio.
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (9/191-192).
[2] Uk. 15.
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
- Imechapishwa: 08/01/2017
al-Halabiy amesema:
“Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy amesema: “Kuhusiana na wengine (Shu´bah, al-A´mash na wengine), nilinukuu maneno ya maimamu waadilifu juu ya kwamba walitumbukia kwenye Bid´ah ikiwa ni pamoja na madhehebu ya Qadariyyah, madhehebu ya Shiy´ah na madhehebu ya Murji-ah. Maimamu wa kujeruhi na kusifu wameyafikisha hayo katika vitabu vyao. Katika wasifu wa kila mmoja nimetaja Bid´ah na kila aliyetumbukia katika Bid´ah hizo na nikataja vyanzo. Maneno yangu ni ya kiuaminifu na hawawezi kuzingatia kuwa nimemtuhumu mtu kiungo.”
Ni pahali gani pa Kishari´ah kunaingia ukanushaji huu wa Shaykh Rabiy´ kwa kitu kilichothibiti kwake? Ninamwacha msomaji mwenye inswafu ajibu swali hili.”
1- Nimetazama vitabu vyangu juu ya yale ambayo al-Haddaad na al-Halabiy wameninasibishia pasi na kupata chochote. Na kama kweli mimi nimesema hivo, basi ninachomuabudu Allaah kwa kukiamini ni kwamba ninamzingatia Shu´bah na Suyfaan ath-Thawriy kuwa ni katika maimamu wa Uislamu ambao ninawapenda na kuwatukuza kwa ajili ya Allaah.
Kuhusiana na al-A´mash (Rahimahu Allaah), alitumbukia katika kitu katika Tashayyu´ lakini ambacho hakikumfanya akawachukia wala kuwasema vibaya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum).
Ama ambao mnaninasibishia kuwa nimesema kwamba wametumbukia katika madhehebu ya Qadariyyah na Murji-ah, nitajieni nao na mninukulie ili niweze kutamka msimamo wangu wa sawa juu yao.
2- Soma maneno aliyosema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):
“Wengi katika Mujtahiduun katika Salaf na waliokuja nyuma walifanya na kusema Bid´ah bila ya kujua kutokana na Hadiyth dhaifu ambazo walidhania kuwa ni Swahiyh, Aayah ambazo walizifahamu kimakosa au maoni yao katika mambo ambayo hawakujua dalili zake. Ikiwa mtu anamcha Allaah vile awezavyo basi anaingia katika Kauli Yake:
رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا
“Mola wetu Usituchukulie tukisahau au tukikosea.” (02:286)
Imepokelewa katika “as-Swahiyh” ya kwamba Allaah amesema:
“Nimefanya hivo.”[1]
3- Umeninukuu katika makala yako ya kwamba nimesema kuhusu Shu´bah:
“Shu´bah ni Imaam mkubwa na bali ni kiongozi wa waumini katika Hadiyth. Ametumia uhai wake katika kufunza na kusomesha Hadiyth na kuwachunguza wapokezi na alisafiri safari ndefu na za usumbufu kwa ajili ya Hadiyth moja.”[2]
Siku zote nimesema hivi na nitaendelea kusema hivo – Allaah akitaka – mpaka nitapokutana Naye.
4- al-Halabiy amesema:
Ni pahali gani pa Kishari´ah kunaingia ukanushaji huu wa Shaykh Rabiy´ kwa kitu kilichothibiti kwake? Ninamwacha msomaji mwenye inswafu ajibu swali hili.”
Ziko wapi dalili zako za wazi ambazo umejengea uthibitishaji huu juu yake?
Uzowefu wangu kwako ni kuwa unaeneza utata juu ya mapokezi ya kiuaminifu kiasi cha kwamba umefikia mpaka kueneza utata juu ya mapokezi ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), jambo ambalo linafanana na usulubu wa Raafidhwah.
Unasema kuwa unawapenda na kuwaheshimu Maswahabah pamoja na kuwa huonelei kuwa ni wenye kutukanwa wakati Sunniy anapowaita “povu” mpaka kuthibiti makubaliano ya kwamba ni tusi. Je, kuna upumbavu na mgongano wenye kutia aibu kushinda huu? Hakuna kimechokufanya kutumbukia kwenye mgongano huu isipokuwa ni matamanio, ushabiki wa kiupofu kwa yule aliyewatukana, mapenzi ya kupitiliza na kumtetea kwa batili.
Hukubali Tabdiy´ ya wanachuoni kwa mtu wa Bid´ah mpaka kuwepo makubaliano juu ya Tabdiy´ hiyo. Hili ni katika misingi yako iloharibika. Sambamba na hilo unakubali maneno ya watu wenye kwenda kinyume na mfumo wa Salaf ambayo baadae unajengea juu yake hukumu yako yenye kugonga. Je, kuna msingi na mgongano ulio mbaya zaidi kuliko huu?
Unajinasibisha na Salafiyyah wakati unatetea gazeti lililo na umoja wa dini, udugu wa dini na uhuru wa dini, ushuhuda wako wa uongo unaposema ya kwamba gazeti hilo limeupambanua Uislamu na kusema kuwa mamia ya watu wapotevu katika Raafidhwah, Khawaarij, Suufiyyah na wengine wenye kulisapoti ya kwamba ni wanachuoni waaminifu na viongozi waaminifu.
Unapenda na kuchukia kwa ajili ya mtu ambaye wazi wazi analingania katika umoja wa dini na unaenda bega kwa bega na watu wenye kulingania katika umoja wa dini na udugu wa dini.
Misimamo yako hii inauvunja Uislamu na Shari´ah kuanzia misingi yake na hujatubu kwa hali yoyote. Pamoja na yote haya wewe na watu mfano wako mnasema kuwa ni Salafiyyuun. Je, kuna mgongano ulio mbaya kabisa na mchafu kushinda huu? Halafu unasema kuwa wengine ndio wenye kujigonga. Mwenye kupeleleza vitabu vyako basi atakuja kuona kuwa wewe ni katika watu wenye kujigonga vibaya sana – mgongano uliojengwa juu ya ujinga na matamanio.
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (9/191-192).
[2] Uk. 15.
Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
Imechapishwa: 08/01/2017
https://firqatunnajia.com/17-al-halabiy-anamtuhumu-rabiy-al-madkhaliy-kumtukana-shubah-ath-thawriy-na-al-amash/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)