Wanazuoni wametaja kuwa watu inapokuja katika kupenda wamegawanyika mafungu matatu:
1 – Wanaopendwa mapenzi safi yasiyokuwa na chuki yoyote. Mapenzi haya yanakuwa kwa Malaika na Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) na waumini maalum, wakiwemo Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum):
وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
“Na wale waliokuja baada yao ni wenye kusema: “Mola wetu! Tusamehe sisi na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo kwa wale walioamini – Mola wetu! Hakika ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.”[1]
Mapenzi kama hayo yanakuwa kwa Salaf na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kutokana na ile ´Aqiydah yao safi na haki na kumtii kwao Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
2 – Wanaochukiwa chuki tupu isiyokuwa na chembe ya mapenzi. Nao ni makafiri ambao ni maadui wa Allaah:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُم مِّنَ الْحَقِّ يُخْرِجُونَ الرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ ۙ أَن تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ رَبِّكُمْ السَّبِيلِ
”Enyi mlioamini! Msimfanye adui Wangu na adui wenu marafiki wandani mkiwapelekea [siri za mikakati] kwa mapenzi na hali wamekwishakanusha haki iliyokujieni. Wanamtoa kwa kumfukuza Mtume pamoja na nyinyi kwa vile tu mmemuamini Allaah, Mola wenu.”[2]
Bi maana watu mnaowapenda, mnaojenga mapenzi kwa ajili yao, mnaowanusuru na kuwatetea. Kilicho cha wajibu ni kujitenga nao mbali, kwa sababu wao ni maadui wa Allaah:
لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ َ
“Hutopata watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake, japo wakiwa ni baba zao, watoto wao, ndugu zao au jamaa zao. Hao [Allaah] amewaandikia katika nyoyo zao imani na akawatia nguvu kwa Roho kutoka Kwake.”[3]
Makusudio ya roho hapa ni nguvu ya imani.
3 – Wanaokusanyiwa mapenzi na chuki. Hili ni kwa muumini mtenda madhami. Anapendwa kwa upande mmoja na anachukiwa kwa upande mwingine. Unampenda kutokana na ile kheri na utiifu alionao, na unamchukia kutokana na yale madhambi na uhalifu anaofanya. Namna hii ndivyo muislamu anatakiwa kupambanua.
Mapenzi jambo lake ni kubwa. Ni lazima kuzinduka na kulijua, kwa sababu sehemu kubwa ya ´Aqiydah na mambo ya dini yanazungukia juu yake. Mtu asitembee kipofu pasi na kujua ni nani anatakiwa kumpenda na ni nani anatakiwa kumchukia. Anatakiwa kufanya kupenda na kuchukia ndio mizani ambayo kwayo anapambanua kati ya wapenzi wa Allaah na wapenzi wa shaytwaan. Asifanye mizani ni mambo ya kidunia na matamanio kwa njia ya kwamba anayeafikiana naye katika mambo yake ya dunia na matamanio yake na pengine akampa kitu katika mambo ya kidunia basi anampenda hata kama atakuwa kafiri na mtenda dhambi mkubwa, na asipompa kitu basi anamchukia hata kama atakuwa ni miongoni mwa watu wema kabisa. Hicho ni kitu kisichojuzu.
[1] 59:10
[2] 60:1
[3] 58:22
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 181-182
- Imechapishwa: 03/12/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 181-182
Imechapishwa: 03/12/2024
https://firqatunnajia.com/167-kupenda-ni-jambo-kubwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)