2 – Mapenzi kwa ajili ya Allaah. Unatakiwa kuyapenda matendo na watu wanaopendwa na Allaah. Unatakiwa kuwapenda waumini na wenye kumcha Allaah:
إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ
“Hakika Allaah anapenda wenye kutubia na anapenda wenye kujitwaharisha.”[1]
Unatakiwa kuwapenda kwa sababu Allaah anawapenda. Wanaochukua nafasi ya mbele kabisa katika watu hao ni Malaika, Manabii, Mitume, mawalii wa Allaah, waja wema na waumini wengine waliosalia. Huku ndio kupenda kwa ajili ya Allaah. Imepokelewa katika Hadiyth:
“Kifungo chenye zaidi cha imani ni kupenda kwa ajili ya Allaah na kuchukia kwa ajili ya Allaah.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mambo matatu yakipatikana kwa mtu hupata utamu wa imani; Allaah na Mtume Wake wawe ni wenye kupendwa zaidi kwake kuliko yeyote yule, ampende mtu na asimpendei jengine isipokuwa iwe ni kwa ajili ya Allaah na achukie kurudi katika ukafiri baada ya Allaah kumwokoa nao kama anavyochukia kutupwa ndani ya Moto.”[3]
Unatakiwa kuwapenda mawalii wa Allaah kwa sababu Allaah anawapenda. Unatakiwa kuwachukia maadui wa Allaah kwa sababu Allaah anawachukia. Kwa hivyo yanakuwa mapenzi na chuki kwa ajili ya Allaah, na si kwa ajili ya mapato ya kidunia. Mja hatoonja utamu wa imani mpaka apende na kuchukia kwa ajili ya Allaah. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:
“Hii leo watu wengi wanajenga udugu kwa ajili ya mambo ya kidunia. Jambo hilo haliwanufaishi chochote wenye kufanya hivo.”
Mapenzi ya kupenda kwa ajili ya Allaah yanabaki duniani na Aakhirah. Kupenda kwa ajili ya mapato ya kidunia hukatika na yanakuwa ni uadui huko Aakhirah:
الْأَخِلَّاءُ يَوْمَئِذٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا الْمُتَّقِينَ
“Marafiki wapenzi Siku hiyo watakuwa maadui wao kwa wao isipokuwa wenye kumcha Allaah.”[4]
Unatakiwa kumchukia mtu kwa ajili ya Allaah na sio kwa ajili amekufanyia vibaya, bali unatakiwa kumchukia kwa ajili ni adui wa Allaah. Hiyo ndio dini ya Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُ مُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ
”Kwa hakika mna kigezo chema kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga mbali nanyi na yale yote mnayoyaabudu badala ya Allaah. Tunakukanusheni na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha ya milele mpaka mumuamini Allaah pekee.”[5]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema mmoja katika wale watakaofunikwa na kivuli siku ya Qiyaamah siku ambayo hakutokuwa na kivuli isipokuwa kivuli Chake, ni “watu wawili waliopendana kwa ajili ya Allaah”[6].
Kupenda na kuchukia kwa ajili ya Allaah ni jambo lenye ngazi ya juu, kwa sababu ni kupambanua kati ya haki na batili:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَتَّقُوا اللَّـهَ يَجْعَل لَّكُمْ فُرْقَانًا
”Enyi mlioamini! Mkimcha Allaah atakupeni Kipambanuo.”[7]
Muumini anatakiwa kuwa na kipambanuzi ambacho anapambanua kati ya haki na batili.
[1] 2:222
[2] Ahmad (18524) na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” (11/215).
[3] al-Bukhaariy (16) na Muslim (43).
[4] 43:67
[5] 60:4
[6] al-Bukhaariy (660) na Muslim (1031).
[7] 8:29
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 179-180
- Imechapishwa: 03/12/2024

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 179-180
Imechapishwa: 03/12/2024
https://firqatunnajia.com/166-kupenda-kwa-ajili-ya-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)