Tunalazimiana na mkusanyiko na tunajiepusha na mambo ya kwenda kinyume. Hatufanyi wala kusema chochote ambacho hakifanywi wala kusemwa na waislamu. Mambo kama hayo yanawatenganisha waislamu na kusababisha uadui kati yao. Maadamu waislamu wanafuata Qur-aan na Sunnah, basi hatutakiwi kuacha yale waliyomo kwa ajili ya maoni yanayoenda kinyume. Mambo ya kwenda kinyume na kutofautiana hayafai. Waislamu ni wenye kufuata haki. Maafikiano yao ni kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ummah wangu haukusanyiki juu ya upotofu.”[1]
Hata Hadiyth ambayo ni Swahiyh inayoenda kinyume na Hadiyth nyingine ambayo ni Swahiyh zaidi ndio inayotakiwa kufanyiwa kazi kwa sababu ile nyingine inazingatiwa ni yenye kwenda kinyume. Kwa ajili hiyo ni lazima kuthibitisha katika jambo hili. Haitakiwi kuchimbua maoni na matendo yaliyoachwa na tukatunga vitabu juu yake na tukawashawishi watu.
Mambo ya kwenda kinyume ni kutofautiana na mkusanyiko wa waislamu. Kutofautiana ni kinyume na kukubaliana. Mipasuko ni kinyume cha umoja. Mambo ya kwenda kinyume ni kinyume na kuungana. Kupekua mambo yanayoenda kinyume ni njia fulani ya kuwatuhumu maimamu upotofu na kuwatia ujingani. Wewe una elimu zaidi kuwashinda? Una elimu maalum ambayo wao hawakuifikia? Hii leo kuna watu wenye kujishughulisha na mambo kama hayo katika jamii ambazo kumeenea ujinga. Mara nyingi mambo hayo hutoka kwa watu wanafunza ambao wanajifanya ni wanazuoni ilihali sio wanazuoni. Hawakusoma ´Aqiydah sahihi na uelewa. Wamejifunza wenyewe na matokeo yake wakawa wanainasibishia dini mambo yasiyostahiki. Hili ni janga. Elimu sio fujo. Elimu inahitaji vidhibiti, uelewa na kufahamu.
[1] Kitaab-us-Sunnah (83). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (83).
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 176-177
- Imechapishwa: 02/12/2024
Tunalazimiana na mkusanyiko na tunajiepusha na mambo ya kwenda kinyume. Hatufanyi wala kusema chochote ambacho hakifanywi wala kusemwa na waislamu. Mambo kama hayo yanawatenganisha waislamu na kusababisha uadui kati yao. Maadamu waislamu wanafuata Qur-aan na Sunnah, basi hatutakiwi kuacha yale waliyomo kwa ajili ya maoni yanayoenda kinyume. Mambo ya kwenda kinyume na kutofautiana hayafai. Waislamu ni wenye kufuata haki. Maafikiano yao ni kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ummah wangu haukusanyiki juu ya upotofu.”[1]
Hata Hadiyth ambayo ni Swahiyh inayoenda kinyume na Hadiyth nyingine ambayo ni Swahiyh zaidi ndio inayotakiwa kufanyiwa kazi kwa sababu ile nyingine inazingatiwa ni yenye kwenda kinyume. Kwa ajili hiyo ni lazima kuthibitisha katika jambo hili. Haitakiwi kuchimbua maoni na matendo yaliyoachwa na tukatunga vitabu juu yake na tukawashawishi watu.
Mambo ya kwenda kinyume ni kutofautiana na mkusanyiko wa waislamu. Kutofautiana ni kinyume na kukubaliana. Mipasuko ni kinyume cha umoja. Mambo ya kwenda kinyume ni kinyume na kuungana. Kupekua mambo yanayoenda kinyume ni njia fulani ya kuwatuhumu maimamu upotofu na kuwatia ujingani. Wewe una elimu zaidi kuwashinda? Una elimu maalum ambayo wao hawakuifikia? Hii leo kuna watu wenye kujishughulisha na mambo kama hayo katika jamii ambazo kumeenea ujinga. Mara nyingi mambo hayo hutoka kwa watu wanafunza ambao wanajifanya ni wanazuoni ilihali sio wanazuoni. Hawakusoma ´Aqiydah sahihi na uelewa. Wamejifunza wenyewe na matokeo yake wakawa wanainasibishia dini mambo yasiyostahiki. Hili ni janga. Elimu sio fujo. Elimu inahitaji vidhibiti, uelewa na kufahamu.
[1] Kitaab-us-Sunnah (83). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (83).
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 176-177
Imechapishwa: 02/12/2024
https://firqatunnajia.com/164-tunalazimiana-na-mkusanyiko-na-tunajiepusha-na-mambo-ya-kwenda-kinyume/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)