Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
131 – Tunafuata Sunnah na mkusanyiko na tunajiepusha na mambo yanayoenda kinyume, kutofautiana na mipasuko.
MAELEZO
Huu ni msingi mkuu miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah; kufuata Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika yule miongoni mwenu atakayeishi muda mrefu basi atakuja kuona tofauti nyingi. Hivyo basi, jilazimieni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza baada yangu. Ziumeni kwa magego yenu. Tahadharini na mambo yaliyozuliwa. Kwani hakika kila kilichozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”[1]
Sambamba na kuamrisha Sunnah, akakataza Bid´ah pia.
Bid´ah ni yale mepya yaliyoingizwa ndani ya dini ambayo hayamo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yeyote atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu atarudishiwa.”[2]
Kila ´ibaadah ambayo mja anajikurubisha kwayo mbele ya Allaah na wakati huohuo ikakosa dalili ndani ya Qur-aan na Sunnah ni Bid´ah. Haijalishi kitu malengo ya mwenye kuifanya ni kujikurubisha mbele ya Allaah, ukweli wa mambo ni kwamba inamweka mbali kabisa na Allaah na halipwi thawabu kwayo. Bali ataadhibiwa kwayo. Sunnah ni ile yenye dalili katika Qur-aan au Sunnah.
[1] Abu Daawuud (4607), at-Tirmidhiy (2676) na Ibn Maajah (34). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2455).
[2] al-Bukhaariy (2697).
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 174-175
- Imechapishwa: 02/12/2024
Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
131 – Tunafuata Sunnah na mkusanyiko na tunajiepusha na mambo yanayoenda kinyume, kutofautiana na mipasuko.
MAELEZO
Huu ni msingi mkuu miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah; kufuata Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika yule miongoni mwenu atakayeishi muda mrefu basi atakuja kuona tofauti nyingi. Hivyo basi, jilazimieni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza baada yangu. Ziumeni kwa magego yenu. Tahadharini na mambo yaliyozuliwa. Kwani hakika kila kilichozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”[1]
Sambamba na kuamrisha Sunnah, akakataza Bid´ah pia.
Bid´ah ni yale mepya yaliyoingizwa ndani ya dini ambayo hayamo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yeyote atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu atarudishiwa.”[2]
Kila ´ibaadah ambayo mja anajikurubisha kwayo mbele ya Allaah na wakati huohuo ikakosa dalili ndani ya Qur-aan na Sunnah ni Bid´ah. Haijalishi kitu malengo ya mwenye kuifanya ni kujikurubisha mbele ya Allaah, ukweli wa mambo ni kwamba inamweka mbali kabisa na Allaah na halipwi thawabu kwayo. Bali ataadhibiwa kwayo. Sunnah ni ile yenye dalili katika Qur-aan au Sunnah.
[1] Abu Daawuud (4607), at-Tirmidhiy (2676) na Ibn Maajah (34). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2455).
[2] al-Bukhaariy (2697).
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 174-175
Imechapishwa: 02/12/2024
https://firqatunnajia.com/162-fuata-sunnah-na-epuka-bidah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)