Baadhi ya watu wanawakaripia wale ambao wanaowaombea du´aa watawala katika Khutbah ya ijumaa. Wanawaita kuwa ni wenye kujikombakomba, unafiki na kujipendekeza. Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu! Huu ndio mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Bali ni katika Sunnah kuwaombea du´aa njema watawala. Watawala wakitengemaa basi na watu pia hutengemaa. Wewe unawaombea du´aa ya kunyooka, kuongoka na kheri. Hata kama kuna mambo mabaya wanayoyafanya, wako na kheri muda wa kuwa bado ni waislamu. Muda wa kuwa wanasimamisha Shari´ah, wanasimamisha adhabu, wanalinda amani, wanazuia mashambulizi dhidi ya waislamu na kuwalinda makafiri dhidi yao, hiyo ni kheri kubwa. Wanaombewa kwa ajili ya mambo hayo. Maasi na madhambi wanayofanya yanawarudilia wao. Lakini wako na kheri kubwa. Wanatakiwa kuombewa kunyooka na kutengemaa. Huu ndio mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Kuhusu wapotofu na wajinga wanaona kuwaombea du´aa watawala ni kujikombakomba na kujipendekeza. Hawawaombei du´aa njema; bali wanawaombea du´aa mbaya.
Wivu hauhusiani na kuwaombea du´aa mbaya. Kama kweli unataka kheri, basi waombee kheri na kunyooka. Allaah ni muweza wa kuwaongoza na kuwarudisha katika haki. Umewakatia tamaa wao kuongozwa? Huku ni kukata tamaa na rehema za Allaah. Isitoshe kuwaombea du´aa ni katika kuwatakia mema. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Dini ni kupeana nasaha.” Tukasema: “Kwa nani, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Kwa ajili ya Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, viongozi wa waislamu na watu wao wa kawaida.”[1]
Huu ni msingi mkuu ambao ni lazima kuuzingatia, na khaswa hii leo.
[1] Muslim (55).
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 172-173
- Imechapishwa: 01/12/2024
Baadhi ya watu wanawakaripia wale ambao wanaowaombea du´aa watawala katika Khutbah ya ijumaa. Wanawaita kuwa ni wenye kujikombakomba, unafiki na kujipendekeza. Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu! Huu ndio mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Bali ni katika Sunnah kuwaombea du´aa njema watawala. Watawala wakitengemaa basi na watu pia hutengemaa. Wewe unawaombea du´aa ya kunyooka, kuongoka na kheri. Hata kama kuna mambo mabaya wanayoyafanya, wako na kheri muda wa kuwa bado ni waislamu. Muda wa kuwa wanasimamisha Shari´ah, wanasimamisha adhabu, wanalinda amani, wanazuia mashambulizi dhidi ya waislamu na kuwalinda makafiri dhidi yao, hiyo ni kheri kubwa. Wanaombewa kwa ajili ya mambo hayo. Maasi na madhambi wanayofanya yanawarudilia wao. Lakini wako na kheri kubwa. Wanatakiwa kuombewa kunyooka na kutengemaa. Huu ndio mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Kuhusu wapotofu na wajinga wanaona kuwaombea du´aa watawala ni kujikombakomba na kujipendekeza. Hawawaombei du´aa njema; bali wanawaombea du´aa mbaya.
Wivu hauhusiani na kuwaombea du´aa mbaya. Kama kweli unataka kheri, basi waombee kheri na kunyooka. Allaah ni muweza wa kuwaongoza na kuwarudisha katika haki. Umewakatia tamaa wao kuongozwa? Huku ni kukata tamaa na rehema za Allaah. Isitoshe kuwaombea du´aa ni katika kuwatakia mema. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Dini ni kupeana nasaha.” Tukasema: “Kwa nani, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Kwa ajili ya Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, viongozi wa waislamu na watu wao wa kawaida.”[1]
Huu ni msingi mkuu ambao ni lazima kuuzingatia, na khaswa hii leo.
[1] Muslim (55).
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 172-173
Imechapishwa: 01/12/2024
https://firqatunnajia.com/160-tunawaombea-duaa-viongozi-wao-wanaomba-dhidi-ya-viongozi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)