Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
38 – Kuonekana ni haki kwa watu wataokuwa Peponi – pasi na kumzunguka wala kulifanyia namna. Kama ilivyotajwa na Kitabu cha Mola wetu:
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ
“Kuna nyuso siku hiyo zitanawiri – zikimtazama Mola wake.”[1]
Tafsiri yake ni kama alivokusudia Allaah (Ta´ala) na kujua. Hadiyth zote Swahiyh zilizopokelewa kuhusu hilo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mambo ni kama alivosema.
MAELEZO
Maimamu wengi, akiwemo mtunzi, wamethibitisha kuwa zipo Hadiyth nyingi zinazothibitisha kuwa waumini watamuona Mola wao siku ya Qiyaamah. Amezitaja baadhi yake kisha akasema:
”Takriban Maswahabah thelathini wamesimulia Hadiyth kuhusu Kuonekana.”[2]
Kisha akasema:
”Kufananisha kumuona Allaah (Ta´ala) kama utavyoonekana mwezi na jua sio kumfananisha Allaah, bali ni kule kuona kwenyewe – na si kile chenye kuonekana. Jengine ni kwamba Hadiyth inathibitisha Allaah kuwepo juu ya viumbe Wake. Vinginvo itawezekanaje kukiona kitu bila kukielekea? Aliyesema kuwa ataonekana pasi na upande wowote basi airejee akili yake. Ima akawa ni mwenye kuifanyia kiburi akili yake au kwenye akili yake kuna kasoro. La sivyo ikiwa anakusudia kuwa hatoonekana si mbele ya yule mwenye kuona, nyuma yake, kuliani mwake, kushotoni mwake, kwa juu au kwa chini, basi ataraddiwa na kila ambaye yuko na maumbile yaliyosalimika.”[3]
[1] 75:22-23
[2] Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (1/217).
[3] Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (1/219).
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 29-30
- Imechapishwa: 18/09/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)