Swali 16: Kuna ambao wanapatwa na aksidenti za gari na mfano wake ambapo inapelekea ubongo kucheza kwa muda wa siku kadhaa au kuzimia kabisa. Je, ni lazima kwa watu hawa kulipa swalah zilizowapita wanapoamka?

Jibu: Ikiwa kipindi ni kifupi, kama siku tatu na chini yake, basi italazimika kulipa kwa sababu kuzimia ndani ya kipindi hiki kilichotajwa kunafanana na kulala. Kwa hivyo jambo hili halizuii kulipa. Imepokelewa kutoka kwa jopo la Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) kwamba walipatwa na kuziria kwa muda ambao haukuzidi siku tatu ambapo wakalipa. Lakini ikiwa muda ni zaidi ya hapo basi hakuna kulipa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu aina tatu; aliyelala mpaka anapoamka, mtoto mpaka anapobaleghe na mwendawazimu mpaka anapopata akili.”

Ambaye amezia ya kipindi kilichotajwa amefanana na mwendawazimu kwa sababu ya kuondokewa na akili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 19
  • Imechapishwa: 16/08/2022