16. Sharti ya swalah – kujisafisha kutokana na najisi

4 – Kujisafisha kutokana na najisi

Mswaliji anapaswa kujisafisha kutokana na najisi katika mwili wake, nguo yake na mahali pake pa kuswalia, isipokuwa najisi iliyosamehewa kama damu kidogo na mfano wake. Ikiwa ameswali akiwa na najisi bila kujua au alijua kisha akasahau, basi swalah yake ni sahihi. Akiijua akiwa ndani ya swalah, basi ataiondoa na kuendelea na swalah yake.

Ardhi yote ni msikiti ambao inasihi kuswaliwa ndani yake, isipokuwa makaburi, bafu, chooni, mazizi ya ngamia na katikati ya njia.

  • Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 23
  • Imechapishwa: 10/10/2026