3 – Kufunika uchi kwa kitu kisichoonyesha ngozi.
Uchi wa mwanamume na mwanamke mtumwa ni kati ya kitovu na goti. Mwili wote wa mwanamke huru ni uchi isipokuwa uso na viganja vyake. Kijakazi ambaye ni mama wa mtoto wa mmiliki wake na mwanamke aliyewekwa huru kwa sehemu ni kama mwanamke mtumwa.
Mwenye kuswali akiwa amevaa nguo iliyoporwa au akiwa katika nyumba iliyoporwa, basi swalah yake haisihi.
Kuvaa dhahabu na hariri kunaruhusiwa kwa wanawake, si kwa wanaume, isipokuwa wakati wa haja. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu dhahabu na hariri:
“Hivi viwili ni haramu kwa wanaume wa ummah wangu na ni halali kwa wanawake wao.”[1]
Mwanamume akiswali ndani ya nguo moja, sehemu yake ikiwa juu ya bega lake, inamtosheleza. Ikiwa hatapata isipokuwa kitu kinachofunika uchi wake, basi aufunike. Ikiwa hakitoshi kuufunika wote, afunike tupu mbili. Ikiwa hakitoshi kuzifunika zote mbili, atafunika mojawapo. Ikiwa atakosa cha kujifunika kabisa, basi ataswali hali ya kuketi chini ambapo ataashiria katika Rukuu´ na Sujuud. Akiswali akiwa amesimama, inajuzu.
Asipopata isipokuwa nguo najisi au sehemu najisi, basi ataswali akiwa katika hivyo viwili. Hatolazimika kurudia swalah yake.
[1] Ahmad (1/96) na (1/115), Abu Daawuud (4057) na an-Nasaa’iy (3595). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Aadaab-uz-Zifaaf”.
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 22-23
- Imechapishwa: 10/10/2026
3 – Kufunika uchi kwa kitu kisichoonyesha ngozi.
Uchi wa mwanamume na mwanamke mtumwa ni kati ya kitovu na goti. Mwili wote wa mwanamke huru ni uchi isipokuwa uso na viganja vyake. Kijakazi ambaye ni mama wa mtoto wa mmiliki wake na mwanamke aliyewekwa huru kwa sehemu ni kama mwanamke mtumwa.
Mwenye kuswali akiwa amevaa nguo iliyoporwa au akiwa katika nyumba iliyoporwa, basi swalah yake haisihi.
Kuvaa dhahabu na hariri kunaruhusiwa kwa wanawake, si kwa wanaume, isipokuwa wakati wa haja. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu dhahabu na hariri:
“Hivi viwili ni haramu kwa wanaume wa ummah wangu na ni halali kwa wanawake wao.”[1]
Mwanamume akiswali ndani ya nguo moja, sehemu yake ikiwa juu ya bega lake, inamtosheleza. Ikiwa hatapata isipokuwa kitu kinachofunika uchi wake, basi aufunike. Ikiwa hakitoshi kuufunika wote, afunike tupu mbili. Ikiwa hakitoshi kuzifunika zote mbili, atafunika mojawapo. Ikiwa atakosa cha kujifunika kabisa, basi ataswali hali ya kuketi chini ambapo ataashiria katika Rukuu´ na Sujuud. Akiswali akiwa amesimama, inajuzu.
Asipopata isipokuwa nguo najisi au sehemu najisi, basi ataswali akiwa katika hivyo viwili. Hatolazimika kurudia swalah yake.
[1] Ahmad (1/96) na (1/115), Abu Daawuud (4057) na an-Nasaa’iy (3595). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Aadaab-uz-Zifaaf”.
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 22-23
Imechapishwa: 10/10/2026
https://firqatunnajia.com/15-swalah-ya-swalah-kufunika-viungo-visivyotakiwa-kuonekana/